Habari za Punde

Serikali ya Awamu ya Nane Imetenga Zaidi ya Bilioni 30 Ili Kutoa Fursa Kwa Makundi Mbalimbali Kujiajiri.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipowasili katika Ofisi za Mahonda kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa Chama wa Mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja (Hawapo Pichani) katika Mkutano maalum uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Chama Mahonda  ambapo amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali ya awamu ya nane itasimamia kwa karibu masuala ya uwezeshaji wa Wananchi.
Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed alioitoa katika Ukumbi wa Ofisi za chama uliopo Mahonda.

Na.Kassim Abdi.OMPR. 

Mjumbe wa Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya awamu ya nane imetenga zaidi ya shiling Billion themanini ili kutoa fursa zaidi kwa makundi mbali mbali kujiajiri kwa kuwawezesha kuwapatia mitaji kwa lengo la kujiajiri.

Mhe. Hemed ameleza hayo wakati akizunhumza na viongozi na wanachama wa mkoa wa kaskazini Unguja katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini zilizopo mahonda.

Amefafanua kuwa, katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa Rais wa Zanzibar na mwenyektii wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteuwa katibu mkuu anesimamia kazi na uwezeshaji kwa lengo la kufanikisha azma ya serikali ya kuwawezesha wananchi wake kupitia makundi mbali mbali.

Akigusia suala la uongozi ndani ya chama Mhe. Hemed amesema CCM imeweka taratibu za kikatiba za kutafuta viongozi na kuwataka viongozi hao kuwa wavumilivu na kuacha kujinadi kwa kupanga safu za uongozi na kusubiri muda ukifika chama kitatangaza taratibu zake.

Kuhusu madawa ya kulevya, Mhe. Hemed aliwaomba viongozi hao kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya nane katika kupambana na kadhia hiyo ili kujenga taifa lenye Afya bora na kupata watendaji bora  wa baadae.

Alifafanua kuwa, Serikali imepanga kuwachukua hatua kali ikiwemo kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria kwa lengo la kuwadhibiti wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu vinavyoiharibu jamii ya wazanzibar.

Katika Kikao hicho Mhe. Hemed aliwataka viongozi wa majimbo kuepukana na  majungu na fitina na badala yake wafanye kazi kwa kushirikiana pamoja kwa kuwashirikisha vingozi wa serikali na Chama katika ngazi zote wakati wakitekeleza majukumu yao.

Mhe. Hemed amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, miiko pamoja na misingi ya chama hicho sambamba na kufanya kazi kwa mashirikiano ili kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Aidha Mhe. Hemed amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kushawishi jamii kuunga mkono juhudi za serikali ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2025

Nae Katibu wa CCM Mkoa wa kaskaizni Unguja Ndugu mula Othamn Zubeir amemueleza Mhe. Hemed kuwa Mkoa huo unasimamia vyema utekelezaji wa Ilani hadi sasa kwa mashikiano ya karibu na serikali ya Mkoa.

Aidha amesema wamefanikiwa kusajili zaidi ya wanachama 25 elfu kwa njia ya elektroniki kwa kutekeleza agizo la chama la kusajili wanachama kwa mfumo huo wa kisasa.

Kwa upande wao wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoa wa kaskazini Unguja walimuelezea makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa kumekuwepo kwa changamoto ya upatikanaji tarjisi za vyeti vya kuzaliwa pamoja na kukosa maji ya uhakika kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kilimo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.