Habari za Punde

Wizara ya Afya yapokea vifaa vya Tiba kutoka Serikali ya watu wa China

Wajumbe kutoka Wizara ya Afya na Ubalozi wa China wakimsikiliza  Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Zhan Zhisheng,  katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa tiba kwa ajili ya Upasuaji wa Ngiri, ambae alishiriki kwa njia ya mtandao huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk.Abdalla Sleiman Ali akizungumza wakati  wa  makabidhiano ya vifaa tiba kwaajili ya upasuaji  wa ngiri vitakavyotumika Hospitali ya Kivunge  Unguja na Chakechake  Pemba,  hafla iliyofanyika  Ukumbi wa Mkutano Hospitali ya Mnazimmoja Mjini Unguja.

 Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk.Abdulla Sleiman Ali, akipokea boksi la Vifaa tiba, vitakavyotumika kwa ajili ya upasuaji wa Ngiri katika Hospitali ya kivunge Unguja na Chakechake kwa upande wa Pemba vifaa hivyo ni msaada kutoka Serikali ya watu wa China.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

 Issa Mzee  - Maelezo     2/09/2021

Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia , na Watoto, imepokea msaada wa vifaa vya upasuaji wa ugonjwa wa Ngiri, vitakavyotumika katika Hospitali ya Kivunge na Chakechake Pemba.

Akizungumza (kwa njia ya mtandao) katika halfa ya kukabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Balozi wa China aliopo Zanzibar, Zhang Zhisheng amesema msaada huo wa vifaa tiba, umetolewa kwa lengo la kuwatibu wananchi wenye tatizo la Ngiri.

Alieleza kuwa, wagonjwa wasiopungua mia moja (100) watanufaika na msaada huo ili kuimarisha afya zao, na kuhakikisha tatizo hilo linaondoka nchini.

Balozi Zhang, amesema Serikali ya watu wa China inaendelea kuisaidia Zanzibar, hasa katika sekta ya afya na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kuisaidia serikali katika kuimarisha afya za wananchi wote.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Abdulla Suleiman Ali, amesema msaada huo utaweza kuwasaidia wagonjwa wasiopungua mia nne, jambo ambalo litapelekea kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa jamii.

Alisema kuwa, misaada mingi inayotolewa na serikali ya China ikiwemo timu za madaktari, vifaa tiba pamoja na dawa ni jambo adimu ambalo lina umuhimu mkubwa  katika kuendeleza na kuimarisha huduma za afya nchini.

Aidha Dk. Abdulla aliupongeza Ubalozi wa china kwa msaada huo na kuahidi kuendeleza ushirikiano baina ya China na Zanzibar kwa maendeleo ya sekta ya afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.