Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt. Mpango Amekutana na Kuzungumza na MD wa Bouygues ya Ufaransa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja  na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson baada ya kumalizika kwa Mazungumzo,Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Oktoba 15,2021.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mzungumzo hayo Eric amesema kampuni  ya Bouygues ina  nia ya kuwekeza katika sekta ya Afya nchini hususan katika Ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa mkoani Dodoma. Aidha, amesema kampuni  hiyo ina uzoefu kwa kutekeleza miradi mikubwa ya  kimataifa katika Bara la Afrika ikiwa imejenga Hospitali katika nchi za Benin, Ghana na Ivory Coast.

Makamu wa Rais , Dkt. Philip Mpango amekaribisha uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini na kuongeza kwamba kutokana na Serikali kuhamia mkoani Dodoma, mahitaji mbalimbali yamezidi kuongezeka hasa katika sekta ya afya. Makamu wa Rais amesema  uwekezaji wa ujenzi wa Hospitali yenye  ubora na vifaa vya kisasa utaongeza tija kubwa kwa wakazi wa Dodoma na mikoa jirani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.