STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.12.2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa
familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki wa aina ya kasa
anayesadikiwa kuwa na sumu huko Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika
salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo
na kuzinasihi familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika
kipindi hichi kigumu cha msiba pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa
haraka waliodhurika baada ya kula samaki huyo.
Rais Dk.
Mwinyi katika salamu hizo za rambirambi, amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kupitia Wizara yake husika itaendelea kuhakikisha wale wote
waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba ili waweze kurudi katika hali zao nzuri
za kiafya.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment