Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Familia na Wananchi katika Kuupokea Mwili wa Marehemi Issa Kassim Issa (Baharia)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika Bandari ya boti za abiria wanaotokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa, aliyefiriki leo 18-12-2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam,akipatiwa matibabu.(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe.Rahma Kassim Ali na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe Simai Mohammed Said

Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwafariji na kutowa mkono wa pole kwa Watoto wa Marehemu Issa Kassim Issa, alipofika Bandari Malindi kwa ajili ya kuupokea mwili wa Marehemi Issa Kassim Issa (Baharia) aliyefariki leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Wanafamilia katika kuupokea Mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyefariki leo 18-12-2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
WANAFAMILIA na Wananchi wakipokea mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) katika bandari ya Malindi Zanzibar baada ya kuwasili na Boti ya Azam Marine, ukitokea Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.