Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Wawekezaji Kutoka Nchini Misri Ikulu Zanzibar.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Makampuni ya Triumph Hotels Group kutoka Nchini Misri, ukiongozwa na Mejor General Ehab Shouman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa mahoteli hayo (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza uamuzi wa Kampuni ya Hoteli za Triumph kutoka nchini Misri wa kuja kuekeza katika sekta ya Utalii hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni hiyo uliongozwa na Meja Jenerali Ehab Shouman ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Hoteli za Triumph kutoka nchini Misri.

Katika mazungumzo yake hayo Rais Dk. Mwinyi umeuhakikishia uongozi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inawawekea mazingira mazuri ili waweze kufikia azma yao waliyoikusudia katika kuekeza kwenye sekta ya utalii.

Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuueleza uongozi huo fursa zilizopo katika uwekezaji kwenye sekta ya utalii  ikiwa ni pamoja na uwepo wa visiwa vidogo vidogo ambapo Serikali imeamua kuviekeza kwenye sekta hiyo.

Aidha, aliueleza uwamuzi huo hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sera ya Uchumi wa Buluu ambayo ndio Dira ya uchumi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliupongeza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la KMKM na Jeshi la Misri na kueleza kwamba azma ya Misri kulisaidia Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) katika mafunzo na mambo mengineyo ya kuimarisha kikosi hicho yatasaidia kwa kiasi kikubwa.

Meja Jenerali Ehab Shouman ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Hoteli za Triumph kutoka Misri kwa upande wake alimueleza Rais Dk. Mwinyi azma ya Kampuni hiyo ya kuekeza hapa Zanzibar katika sekta ya utalii na kueleza jinsi walivyovutiwa na mazingira pamoja na mikakati ya uwekezaji iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Mwinyi..

Nae Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM), Komodoo Azana Hassan Msingiri alieleza mashirikiano mazuri yalioopo kati ya kikosi hicho na uongozi huo na kupongeza azma ya Misri ya kukisaidia kikosi hicho ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo kwa kikosi chake ili kuimarisha Sera ya Uchumi wa Buluu sambamba na kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji hao hapa  Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega Uchumi (ZIPA) Sharif Ali Sharif  alisema kuwa ugeni huo umekuja kwa azma ya kufanya mashirikiano na Serikali kupitia Kikosi cha (KMKM) na kuonesha nia ya kuekeza kwa kujenga hoteli yenye nyota tano, kuekeza katika uvuvi pamoja na miundombinu ya ujenzi wa viwanja vya ndege.

Kitengo cha Habari


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake Mkuu wa Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Nchini Misri wa Makampuni ya Triumph Hotels  Mejor General Ehab Shouman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Mahoteli ya Triumph, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Makampuni ya Triumph Hotels Group kutoka Nchini Misri, ukiongozwa na Mejor General Ehab Shouman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa mahoteli hayo (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mejor General Ehab Shouman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Mahoteli ya Triumph Hotels Group.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu na ujumbe wake kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-12-2021, (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.