Na Mwandishi wetu, Roma
Wawekezaji zaidi ya 140
kutoka Italia wamewekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania
Takwimu hizo zimetolewa na
Naibu Waziri Wizara ya Madini, Prof. Shukrani Manya alipokuwa akifungua jukwaa
la biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lilifanyika Jijini Roma,
Italia leo.
Prof. Manya amasema kuwa
miradi hiyo inathamani ya Shilingi bilioni 5 inayotoa ajira kwa watanzania
zaidi ya 4000.
“Jukwa hili tunataka
liendelee kuwa sababu ya kuchagiza uwekezaji mwingine kutoka Italia kwa kutumia
teknolojia waliyonayo, kwa kutumia utalaamu walionao wa designing na …….na sasa
waone kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na Tanzania inaendelea kuweka
mazingia wezeshe ya kukuza sekta ya uwekezaji na biashara,” Amesema Prof. Manya
Ameongeza kuwa kupitia
jukwaa la biashara na uwekezaji biashara na uwekezaji utaendelea kuongezeka na
kuongeza zaidi na hasa katika maeneo ambayo tumawaeleza hapa kupitia jukwaa
hili.
Kwa upande wake Balozi wa
Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo amesema kuwa kufanyika kwa
kongamano hili la biashara na uwekezaji lengo lake kubwa ni kuwavutia
wafanyabiashara na wewekezaji wa sekta mbalimbali kutoka Italia kuwekeza zaidi
Tanzania.
“mwitukio ni mkubwa na
tumeitikiwa na jumuiya za kibiashara na wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya
250 kutoka nchi zote mbili wameshiriki katika kongamano hili,” amesema Balozi
Kombo
Balozi Kombo ameongeza
kuwa, Wafanyabiashara kutoka italia ni wabobezi katika sekta ya madini lakini
pia katika utalii hivyo ni matumanini yake kuwa mara baada ya kumalizika kwa
kongamano hilo wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Italia wataongezeka zaidi
Tanzania.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Chama Wawekezaji katika Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo Rosso
amewasihi wawekezaji kutoka Italia kuwekeza kwa wingi Tanzania kwa kuwa
mazingira ya biashara na uwekezaji ni tulivu na salama.
“Tanzania ni sehemu salama
kuwekeza…..nawahakikishia mimi nimewekeza Tanzania na ninaona ni sehemu salama
ya kuwekeza karibuni sana kuwekeza kwa maendeleo ya Tanzania na Italia,”
amesema Bw. Rosso
Nae Mkurugenzi wa Idara ya
Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ameongeza kuwa katika kutekeleza maelekezo
ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Wizara ya
Mambo ya Nje inatekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuhakikisha uchumi
unaongezeka.
Jukwa hilo la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limehudhuriwa na Wafanyabiashara na
Wawekezaji takribani 250 kutoka nchi zote mbili.
Wafanyabiashara na
wawekezaji hao ni wa sekta za utalii, kilimo, madini, na ujenzi.
Pamoja na mambo mengine,
jukwaa hilo limewawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, uwezekano
wa ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya biashara na njia ya kuboresha
mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Italia kwa kushirikiana na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Mamlaka ya Taifa ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
No comments:
Post a Comment