Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameondoka Unguja kuelekea Kisiwani Pemba Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa Uzinduzi wa Miradi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kikazi ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba.  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili kisiwani Pemba leo kwa ziara ya kikazi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah ambapo baada ya kuwasili kisiwani humo akiwa amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi alipokewa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor Masoud.

Akiwa kisiwani Pemba, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi hapo kesho (Januari 03.2022) mapema asubuhi anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar huko Konde, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi baada ya shughuli hiyo anatarajiwa kuwasili Kinyasini Wete kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi Kiwanda cha kutengeneza Maji Safi Watercom (T) Ltd na baadae kuwahutubia wananchi.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.