Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi awasili Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake UAE

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiagana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania U.A.E Balozi Mohammed Abdalla Mtonga, katika Uwanja wa Ndege wa Al Bateen Abu Dhabi, baada ya kumaliza ziara yake ya Kiserikali ya Siku Tatu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (U.A.E) baada ya kumaliza ziara yake ya siku Tatu ya Kiserikali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Viongozi wa Serikali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea katika Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) baada ya kumaliza ziara yake ya Kiserikali ya Siku Tatu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, baada ya kuwasili Zanzibar na  kuzungumzo na Waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake (U.A.E) na  (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora.Mhe.Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk.(Picha na Ikulu)
MWANDISHI wa Habari  wa ITV na Nipashe Zanzibar Bw., Farouk Karim akiuluza suali wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) kuhusiana na ziara yake (U.A.E) (Picha na Ikulu)
WAANDISHI wa Habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) uliofanyika katika Ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, baada ya kuwasili Zanzibar akitokwa Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na ziara yake katika Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu(U.A.E) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea Umoja ya Nchi za Falme za Kiarabu baada ya kumlaliza ziara yake ya siku tatu. Na (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Serikali baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, uliofanyika katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.