Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma
wakati akiondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma kuelekea Kampala Nchini
Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Februari 1,2022.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA MAKAMU WA RAIS
Anwani
ya simu:“MAKAMU”, Mji
wa Serikali,
Simu
Na.: +(255)026 2329006 Eneo
la Mtumba,
Nukushi.:
+(255)026 2329007/2983150 S.
L. P. 2502,
Barua
Pepe: km@vpo.go.tz 40406 DODOMA,
TANZANIA.
01 Februari 2022
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 1 Februari 2022 ameondoka nchini kuelekea Kampala nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Akiwa nchini Uganda Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kutoa maamuzi ya mwisho ya uwekezaji (Final Investement Decision) katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani nchini Tanzania (EACOP).
Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika katika uwanja wa sherehe wa Kololo uliopo Kampala Uganda na kuhudhuriwa na makampuni mbalimbali ya kimataifa ambayo ni wabia wa mradi huo.
Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu
wa Rais - Habari.
No comments:
Post a Comment