Habari za Punde

Taqwa Ophrans Trust yaandaa kongamano la kuchangisha futari kwa ajili ya mayatima



Wajumbe katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima wanaoishi majumbani wakifuatilia kongamano la kuchangisha futari kwaajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taasisi ya kusaidia mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu akizungumza katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto yatima waishio majumbani huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar,hafla hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kusaidia watoto mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust.

Mwenyekiti wa Taasisi ya kusaidia mayatima waishio majumbani Tanzania Taqwa Ophrans Trust  dkt. Salha Mohammed  Kassim akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar mama Zainab kuzungumza na kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto mayatima waishio majumbani,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Wajumbe katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima wanaoishi majumbani wakifuatilia kongamanola kuchangisha futari kwaajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taasisi ya kusaidia mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu (kulia) Akimkabidhi picha maalum mwenyekiti wa  Taasisi ya kusaidia mayatima waishio majumbani Tanzania Taqwa Ophrans Trust ambayo aliinunua mweneyekiti huyo Kwa thamani ya shilingi laki 5 ya kitanzania ikiwa ni mchango wake katika kusaidia futari kwaajili ya  mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari  Kwa ajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taqwa Ophrans Trust huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwandishi wa habari gazeti la Zanzibar Leo Juma Mmanga akiendesha zoezi la kuuza Kwa mnaada ikiwa ni Harambee kuchangisha futari kwa ajili ya watoto mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima hao lililofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu (katikati) akipokea picha maalum kutoka kwa mshereheshaji wa mnada Juma Mmanga mara baada ya kuinunua picha hiyo Kwa thamani ya shilingi milioni moja ya  kitanzania ikiwa na mchango wake Kwa ajili ya futari ya watoto mayatima waishio majumbani wakati wa kongamano la kuchangisha futari  Kwa ajili ya watoto hao lililofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege  Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.
Na Khadija Khamis – Maelezo  Zanzibar 

Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zainab Kombo  amewataka waislamu pamoja na wapenda furaha na faraja kujitokeza kuiunga mkono Taasisi ya Taqwa Orphans Trust Tanzania , kwa kutoa ufadhili na kudhamini watoto yatima wanaowasimamia  kwa lengo la kuwajengea  uwezo madhubuti wa kuwahudumia vijana hao.


Akiyasema hayo  katika Ukumbi wa Gorden Tulip wakati wa kongamano la kuchangisha Iftar kwa watoto yatima  waishio  Majumbani mwao.

Amesema  jamii iendelee kushajihishana  kutoa  hasa katika  kipindi cha Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani  na  si kwa Taasisi ya Taqwa pekee bali na  Taasisi nyengine zinazoshughulikia Watoto yatima  kufanya hivyo kutasaidia kuwapa faraja na ni njia moja wapo ya kufanya biashara na  Mola Muumba hakika biashara hii haina hasara


Mama  Zainab amesema atahakikisha anashirikiana na Taasisi hiyo, hatua  kwa hatua  katika kufanikisha  shughuli za kila siku za kuwahudumia vijana hao.


Aidha amesema  amefurahishwa  kwa fikra ya kuanzisha taasisi hii ambao imesimamiwa na kutekelezwa na wanawake kwa hakika  wanawake hao  sio chemchem ya upendo na huruma bali ndio walezi wa jamii hii,na ni kimbilio la wenye dhiki na waliokosa furaha na pia ni mbegu bora ya amani katika nchi yetu.


Nae Mwenyekiti na Taqwa Orphans Trust Tanzania  Dr Salha Mohamed Kassim alisema lengo la Jumuiya hii  ni kuwapa furaha watoto yatima walio majumbani mwao kwa kuwapatia huduma  za msingi za kijamii ikiwemo  chakula, huduma za afya, elimu pamoja na shughuli za Iftar kwa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani.


Alifahamisha kwamba Taasisi ilifanya utafiti wa kujuwa jinsi ya kuwapa malezi bora yenye furaha watoto yatima wakagundua kwamba ni kuishi na familia zao zenye udugu wa damu ndio watapata faraja zaidi kuliko kuwatenga .


“ Malezi na Makuzi bora kwa watoto yatima ni kuishi na familia zao zenye udugu wa damu ambazo zinaleta upendo  na  faraja  na  ni silaha muhimu ya watoto pamoja na kufuata mila  silka na tamaduni  zao  jambo ambalo linajenga imani kubwa kwa watoto hao na kuridhika , kuliko kuwatenga “alisema Dr Salha.


Akitoa wito kwa waumini  kujitokeza kwa wingi kuwachangia watoto hao kwa ajili ya kuitafuta kheri ya hapa duniani na kesho ahera hata kwa kitu kidogo  mtu ulichonacho kitasaidia  .


Taasisi ya  Taqwa Orphans Trust Tanzania  imeanzishwa na wanawake  wa kiislamu katika mwaka 2011 na Makao Makuu  yake yapo  Dar-es –salamu, hadi sasa wameweza kufikisha futari kwa  familia  1593.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.