Habari za Punde

Kishindo cha Mhe.Membe Kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Shaka Aongoza Mapokezi.

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka HAMDU Shaka akimkabidhi ya CCM,aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha ACT Wazalendo, Bernard Membe aliyerejea CCM, katika Mkutano wa mbunge jimbo la Mtaka, Nape Nnauye katika Kijiji cha Rondo, Mtaka mkoani Lindi (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Aliyewahi kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ameeleza sababu zilizomfanya arejee CCM ikiwemo kuondoka kwa sababu ambayo ilimfanya atimkie upinzani.
Aidha, amefunguka jinsi alivyoumia kutokana na uamuzi wa kumwondolea uanachama wa CCM, Chama alichokulia huku akiahidi sasa atafia ndani ya CCM.
Akizungumza katika mkutano huo, katika Kijiji cha Rondo, alisema Machi 30 hadi Aprili 1, mwaka huu aliitwa Dodoma, kwenye kikao cha kamati ya Maadili ya CCM Taifa na Vikao vya kamati kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ambapo kote alipewa nafasi na Mwenyekiti wa CCM Taifa kuzungumza na wajumbe wa vikao hivyo juu ya kurejeshewa uanachama wake.
“Mama yetu, Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa  CCM Taifa Ndugu Samia Suluhu Hassan alinipa nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa kamati kuu ya Chama Taifa. Nashukuru kwa kupewa nafasi ile na wajumbe waliliridhia kwa kauli moja nirejee CCM. 
Nimerejea CCM kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza nilishauriwa na viongozi wa dini zote, nilishauriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkoa, nilishauriwa na marafiki zangu wote nirejee CCM, nilishauriwa na wana CCM.
Kutokana na ushauri wote huo sikuwa na namna nyingine zaidi ya kutii, nimekubaliana na ushauri wa wote waliosema nirudi CCM na sasa nimerudi CCM,” amesema Membe.
Amesema sababu ya pili ya kurudi kwenye Chama hicho inatokana na dhamira yake ya kukitumikia Chama Cha Mapinduzi hadi atakapokwenda kaburini. “Nilipoondolewa CCM nilisikitika sana, nilisononeka sana, na ninyi wananchi mlisikitika na mlisononeka sana."
“Sababu ambazo zilinifanya niondoke CCM haziko tena, narudi sababu zilizoniondoa CCM haziko tena. Nimerudi, namshukuru Mwenyekiti wa CCM Mama yetu Samia Suluhu Hassan, wajumbe wa Kamati Kuu na halmashauri Kuu ya Taifa kwa  kunirudisha. Nimerudi kwenye Chama ambacho nimezaliwa na kukulia, chama ambacho kimenisomesha na kunipa heshima ya kutumikia Nchi yangu,-Membe.@ccmtanzania @shakazulu36.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha ACT Wazalendo, Bernard Membe anayebusu kadi ya CCM baada ya kukabidhiwa na Shaka katika Mkutano wa mbunge jimbo la Mtaka, Nape Nnauye katika Kijiji cha Rondo, Mtaka mkoani Lindi


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipokipokea Kadi za Wanachama zaid ya 1600 Walio rejesha kadi za Vyama Vya Upinzani katika Mkutano wa mbunge jimbo la Mtaka, Nape Nnauye katika Kijiji cha Rondo, Mtaka mkoani Lindi (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka HAMDU Shaka akimkaribisha CCM, aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha ACT Wazalendo, Bernard Membe aliyerejea CCM, wakati wa Mkutano wa mbunge jimbo la Mtaka, Nape Nnauye katika Kijiji cha Rondo, Mtaka mkoani Lindi 


Attachments area

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.