Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe
22 Juni, 2022 akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kigali nchini Rwanda
ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Serikali wa
Nchi Wanachama za Jumuiya ya Madola.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA MAKAMU WA RAIS
Anwani
ya simu:“MAKAMU”, Mji
wa Serikali,
Simu
Na.: +(255)026 2329006 Eneo
la Mtumba,
Nukushi.:
+(255)026 2329007/2983150 S.
L. P. 2502,
Barua
Pepe: km@vpo.go.tz 40406 DODOMA,
TANZANIA.
Kigali, Rwanda
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe
22 Juni, 2022 amewasili Kigali nchini Rwanda ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 26 wa
Wakuu wa Serikali wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Madola.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 24 na 25 Juni 2022 Jijini Kigali nchini Rwanda ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo Mabadiliko ya tabia ya nchi, Uvumbuzi na teknolojia , Biashara, Vijana, Utawala bora , Afya pamoja na kukabiliana na athari za Uviko 19.
Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu
wa Rais - Habari
No comments:
Post a Comment