Habari za Punde

Viongozi Wakubwa Waaza Kuonesha Njia Wakubali Kuhama kwa Hiari Ngorongoro. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mongela Apongeza Uamuzi Huo.

Kapteni wa Jeshi Mstaafu na  ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne, Mhe. Kaika Ole Telele akizungumza na Waandishi wa habari  akielezea kuwa ameamua kufanya maamuzi ili kuonesha yeye sio kikwazo katika mpango huo wa serikali wa kuhamisha wananchi kwa hiari katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Mazungumzo hayo yamefanyika katika Kijiji cha Enduren kilichopo wilya Ngorongoro mkoani Arusha.
Kapteni wa Jeshi Mstaafu na  ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne, Mhe. Kaika Ole Telele akiwa ameshikilia bango wakati tathmini ikifanyika katika moja ya nyumba zake kwa ajili ya kulipwa fidia mara baada ya kukubali kuhama kwa  hiari katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi, 


Na Mwandishi wetu, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John Mongela  ametaja majina ya Viongozi wakubwa wa kwanza waliokubali kuhama katika  Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga kuungana na wananchi wengine ambao wameshahamia. 

Ameweka wazi majina hayo leo Jijini Arusha wakati  akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea tathmini ya  muendelezo wa awamu ya tatu ya  wananchi waliokubali kuhama katika eneo hilo na kwamba kundi hilo lenye kaya 25 litaanza safari Alhamisi ya wiki hii.

Ametaja majina hayo akiwemo aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo Ngorongoro Mkoani Arusha, Mhe. Kaika Ole Telele, Diwani wa kata ya Eyasi, Augustino Lukumay, Diwani wa Viti maalum wa Kata ya Eyasi Mhe. Veronica Litiga pamoja na Kiongozi wa Kabila la Wadatoga.

Mhe.Mongela amesema hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika mchakato huo na kubainisha kuwa Viongozi hao kwa pamoja  wamekiri kuwa wapo tayari kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera kwa lengo la kupisha shughuli za Uhifadhi.

Ameongeza kuwa viongozi hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii hiyo wamesema ikiwa wao ni viongozi wameamua kuchukua uamuzi huo ili kuonesha njia kwa wananchi wengine ili waanze kujitafakarikuhama katika eneo hilo lenye maslahi makubwa kwa  taifa.

Kwa upande wake Kapteni wa Jeshi Mstaafu na  ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne ameeleza kuwa ameamua kufanya maamuzi ili kuonesha yeye sio kikwazo katika mpango huo wa serikali wa kuhamisha wananchi kwa hiari.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Eyasi, Mhe, Augustino Lukumay ameeleza uamuzi huo wa serikali ni wa busara na kwamba ni muda muafaka kwao wananchi wa Ngorongoro kuanza  kumiliki nyumba, ardhi na kujishugulisha na shughuli za kiuchumi ambazo tokea kuzaliwa kwao Ngorongoro hawakuwahi kuzipata  ila kwa sasa Msomera wanakwenda kuwa na haki hizo kama ilivyo kwa watanzania wengine.

Kwa upande wake Diwani wa viti maalum wa  Kata ya Eyasi, Veronika Litiga amelezea kuwa yeye kama kiongozi ameamua kuonesha njia na kwamba hatua hiyo ya serikali ya kuhama kwa hiyari katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kwa kuwa yeye ni mwanachama wa chama hicho ni lazima aweze kuitikia wito huo wa serikali

''Ninakwenda Msomera nikiwa na amani kwa vile naamini Chama changu na serikali yangu haiweze kunipeleka mahali ambako ni kubaya naamini Msomera ni mahali bora kwa ajili ya wanangorongoro walioteseka kwa muda mrefu kwa kukosa haki ya kuendesha shghuli za kiuchumi katika eneo la Uhifadhi'' Alisisitiza Diwani wa Viti Maalum wa Kata ya Eyasi, Veronika Litiga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.