Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aendelea na Ziara Yake Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "A"Unguja na Kupokea Taarifa ya Utendeji Kazi ya Mkoa Huo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Viongozi wa Serikali na Chama wa Mkoa wa Kaskazini Unguja alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni kwa ajili ya kupokea taarifa ya Mkoa kabla ya kuaza kwa ziara yake iliyofanyika leo 19-7-2022, katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja kabla ya kuaza kwa ziara hiyo iliyoazia katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 19-7-2022, kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mkoa huo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni,(kulia kwa Rais ) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akiwasilisha taarifa ya utekelezaji  wa Miradiu ya Maendeleo ya Mkoa wake wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuo wa Mkoa, kabla ya kuaza kwa ziara  yake katika  Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Viongozi wa Serikali wakifuatilia taarifa ya utekeleza ya Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati ikiwasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwasilia kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Mkokotoni,  kabla ya kuaza kwa ziara yake katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja
BAADHI ya Mawaziri wakifuatilia taarifa ya utekelezaji ya Miradi ya Maendelo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(hayupo pichani)  kabla ya kuaza kwa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi , katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.