Habari za Punde

Mwenyekiti wa TLP Augustino Lyatonga Mrema Amefariki Dunia Leo 21-8-2022.

 Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.

Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro na amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.