Habari za Punde

Balozi Sokoine Amekutana na Kuzungumza na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ya Saudi Arabia

Kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza ushirikiano baina ya pande hizo mbili ambapo Saudi Arabia imeonyesha utayari wa kujadiliana na Serikali ya Tanzania kuhusu masuala ya upatikanaji wa viza za kuingia nchini Saudi Arabia.

Kwa upande wake, Balozi Sokoine ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wake kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Balozi Sokoine ametumia mazungumzo hayo kuelezea utayari wa Tanzania kuingia makubaliano ya kuanzishwa Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya nchi hizi mbili katika kusimamia utekelezaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya akieleza jambo wakati wa kikao chake na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Ujumbe wa Saudi Arabia ukiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Luteni Generali Suliman Al-Yahya ukijitambulisha wakati wa kikao baina yake na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine  
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Saudi Arabia


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.