Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres kabla ya mazungumzo yao yaliofanyika
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro
unaopatikana nchini Tanzania Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio
Guterres mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa Jijini New York nchini Marekani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo (Tete a tete ) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres , Mazungumzo yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.
Hii leo tarehe 22 Septemba 2022 Makamu wa Rais akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaondelea nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment