Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki na Kuhutubia katika Tamasha la Kizimkazi, Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi mara baada ya kuwasili katika eneo la Kizimkazi Dimbani kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la Kizimkazi  tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa na vifaa vya matumizi ya aina mbalimbali katika mabanda ya Maonesho kwenye kilele cha   Tamasha hilo  la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa mbalimbali vya Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar KMKM wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye Tamasha la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Kiazi Kikuu kilichochimbuliwa kwenye ardhi kavu na Wazee wa Jadi kutoka Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi katika Siku ya kilele cha Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022

 Wataalam wa Jadi wa Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi wakionesha uwezo wa kufanya vitu mbalimbali wakati wa Sherehe za Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.