Msanii maarufu katika kughani mashairi nchini
Tanzania Mrisho Mpoto, maarufu 'Mjomba’ akitumbuiza wakati wa hafla ya ufunguzi
wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki
(JAMAFEST) Septemba 5, 2022 2022 ambalo linafanyika katika Uwanja wa Michezo wa
Intwari Bujumbura, nchini Burundi.
Na.Eleuteri Mangi-WUSM
Tanzania inashiriki Tamasha la Tano la Sanaa na
Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) 2022 ambalo linafanyika
nchini Bujumbura Burundi likiongozwa na Kaulimbiu “Kutumia Rasilimali za
Kiutamaduni kukabiliana na Athari za UVIKO-19 kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki”.
Akifungua tamasha hilo Septemba 5, 2022 katika Uwanja wa Intwari Bujumbura nchini humo, Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye amewashukuru Wakuu wa nchi za jumuiya hiyo kufanikisha vikundi vya Utamaduni na Sanaa kushiriki Tamasha la JAMAFEST 2022 kwa mafanikio nchini Burundi.
“Tukio hili husaidia sio tu ubadilishanaji wa kisanii na kitamaduni, lakini pia hukuza ushirikiano wa kikanda. Kuweza kuandaa tamasha hili la Sanaa na Utamaduni nchini Burundi, ni dalili tosha kwamba UVIKO 19 ipo nyuma yetu ushahidi kwamba jumuiya yetu ni thabiti na kwa pamoja tunaweza kukabiliana na changamoto yoyote” amesema Rais Mhe. Ndayishimiye.
Awali akiwakaribisha washiriki wa tamasha hilo Rais Mhe. Ndayishimiye, amesema kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema wafurahie sio tu hewa ya Burundi, bali watafurahia madhari nzuri ya Ziwa Tanganyika, kula samaki aina ya mgebuka,dagaa na kuhe ambao wanapatikana katika ziwa Tanganyika.
Aidha, Rais Mhe. Ndayishimiye amesisitiza umuhimu wa Tamasha hilo na kusema kuwa linanaongeza kuimarisha umoja na muingiliano kati ya watu wa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tamasha la JAMAFEST linafanyika kwa mzunguko ambapo
mwaka 2022 ni zamu ya nchini Burundi baada ya kufanyika tamasha la 4 kufanyika
kwa mafaniko makubwa jijini Dar es Salaam 2019.
Vikundi vya ngoma wakitumbuiza wakati wa hafla ya
ufunguzi wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (JAMAFEST) Septemba 5, 2022 2022 ambalo linafanyika katika Uwanja wa
Michezo wa Intwari Bujumbura, nchini Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste
Ndayishimiye akifungua Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya
Afrika Mashariki (JAMAFEST) Septemba 5, 2022 2022 ambalo linafanyika katika
Uwanja wa Michezo wa Intwari Bujumbura, nchini Burundi.
Washiriki wa Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) Septemba 5, 2022 2022 ambalo linafanyika katika Uwanja wa Michezo wa Intwari Bujumbura, nchini Burundi.
No comments:
Post a Comment