Habari za Punde

Kikao cha ushirikiano baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar chafanyika Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Dkt. Islam Salum akizungumza wakati wa kikao cha Ushauriano baina ya ofisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Oktoba 13, 2022 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa shughuli zinazotekelezwa na ofisi hizo kwa pande zote mbili.
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Dkt. Islam Salum wakati wa kikao cha Ushauriano baina ya ofisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Oktoba 13, 2022 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Leonard Mchau (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Pascal Vyagusa (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu muundo wa majukumu ya Ofisi hiyo wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Bi. Lilian Francis (kushoto aliyesimama) akiwasilisha taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Idara ya Kazi wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Rashid Maftah (kulia) akiwasilisha taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na kitengo hicho wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.