Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Uswizi nchini, Mhe. Didier Chassot wakizindua Madawati ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Katika Wizara za Kisekta baada ya Waziri Mkuu kuhutubia kwenye Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali lililofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto mwenye ulemavu Chipowenga Zayeye, wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima na wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi, katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Msaada wa Kisheria (LSF) Lulu Ng’wanakilala kuhusu machapisho mbalimbali yanayotolewa na Asasi hiyo katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma , Oktoba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Doroth Gwajima Tuzo kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022. Katikati ni Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza kulia ni Mwenyekiti wa NaCONGO, Dkt. Lilian.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment