Habari za Punde

MPINA AREJESHA FOMU YA KUOMBA UNEC WA CCM MKOA WA SIMIYU NA UNEC CCM VITI 15 TANZANIA BARA

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Mohammed Ali Khalfan akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Joelson Mpina fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya MNEC Mkoa wa Simiyu na MNEC Viti 15 Tanzania Bara Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi

MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Joelson Mpina amechukua na kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Mkoa wa Simiyu pamoja na kuomba nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara.

Mpina amerejesha fomu hizo Oktoba 5, 2022 saa 9;50 alasiri katika Ofisi Kuu ya CCM, Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi na kupokelewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Mohammed Ali Khalfan.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Shaka Hamdu Shaka zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi ya NEC Mkoa na Taifa imefikia mwisho Oktoba 5, 2022.


Mmoja wa waasisi wa TANU sasa CCM kutoka Kijiji cha Mwandu-Itinje wilaya ya Meatu, Mzee Bugalama Ng'ondi akifuatia zoezi la makabidhiano ya fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya MNEC Mkoa Simiyu na MNEC Viti 15 Tanzania Bara kwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina hayuko pichani kushoto ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Meatu, Mota Mpina
Baadhi ya viongozi wa CCM Kata na matawi kutoka Jimbo la Kisesa Wilaya Meatu wakifuatilia kwa makini zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa Mbunge wa Kisesa Luhaga Joelson Mpina Oktoba 5, 2022 Bariadi Simiyu.
Katibu wa Chama Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Mohammed Ali Khalfan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na ujumbe wake aliombatana nao baada ya kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya MNEC Mkoa wa Simiyu na MNEC Viti 15 Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.