Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aendelea na Ziara Yake Nchini Oman Ikiwa Siku ya Pili leo 12-10-2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi,  leo Jumatano  tarehe 12 Oktoba 2022 ameingia siku ya pili ya ziara yake nchini Oman, ambapo baada ya kukutana na Mtawala wa Oman Mh. Sultan Haitham bin Tariq kwa mazungumzo yaliyofanyika katika Kasri la Sultani la Al Barakah alielekea kutembelea Msikiti Mkubwa unaojulikana kama Grand Mosque ambapo alitembezwa na kushuhudia maajabu ya ukubwa wa Msikiti huo unaovutia.

 Ziara yake ya leo iliyojaa harakati nyingi ilimchukua hadi katika majengo yanayohifadhi nyaraka mbalimbali za kale zikiwemo za Zanzibar  eneo limaloitwa GHALA.

 Baada ya hapo akaelekea  katika jengo kubwa la Kifalme linalotumika kwa ajili ya maonesho ya muziki na sanaa. Ni jengo la kisasa kwa wale wanaovutiwa na sanaa za maonesho.

Baadae alitembelea Jumba la Makumbusho ya Taifa liitwalo Oman National Museum.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.