Habari za Punde

Mhe Hemed akutana na Watendaji wa Idara ya Uratibu za Shughuli za SMZ Dodoma

Watendaji wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Dodoma wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alipofika Ofisi za Idara hiyo zilizopo Dodoma  kukagua na kujua uendeshaji wa Ofisi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla (wa kati) akiwa na Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, uratibu wa Baraza la wawakilishi Dkt. Islam Seif Salum (Kulia) wakiwa katika Picha ya pamoja na Watendaji wa Idara ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dodoma wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo Ndg. Khalid Bakari Hamran

Na Abdulrahim Khamis 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezitaka Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusimamia Matumizi ya Fedha za Serikali ili kurejesha heshima ya Fedha Nchini.

Mhe. Hemed ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Idara ya Uratibu za Shughuli za SMZ Dodoma alipokutana nao Afisini kwake Dodoma.

Ameeleza kuwa Taasisi nyingi za Serikali baadhi ya huduma husita kwa kisingizio cha ukosefu wa Fedha ambapo baadhi ya maeneo huhitaji Busara na Maamuzi sahihi katika Matumizi.

"Tumeimarisha na tutaendelea kusimamia usimamizi wa Fedha za Serikali lengo tunataka fedha za Serikali ziheshimiwe kuna  maeneo tatizo sio Fedha bali ni Matumizi ya Fedha"

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kufurahishwa kwake kuona Watendaji wa Idara hiyo wanawajibika ipasavyo licha ya changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo.

Amefafanua kuwa ni dhahiri Juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni zinaonekanwa na wengi ambapo ameahidi kuwa Ofisi kuwa ya mwanzo kuunga Mkono Juhudi hizo.

Amesema Rais Dkt. Mwinyi ameudhirishia umma wa Wazanzibari kuwa amedhamiria kutatua Changamoto zinazowakabili Wafanyakazi hasa suala la Maslahi na kuongeza kuwa Changamoto nyengine za Wafanyakazi ameshatoa Maelekezo ili wafanyakazi wawe na Mazingira Rafiki ya uwajibikaji.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Idara hiyo kwa kuendeleza mashirikiano baina yake na Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hatua ambayo itawarahisishia Maraisi  wote wawili kuweza kutumiza malengo yao ya kuwatumikia Wananchi wao.

Kuhusu uendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Dodoma Mhe. Hemed amefurahishwa na hatua ya Benki hiyo kufungua Tawi Jijini Dodoma eneo ambalo ndio Makao Makuu ya Tanzania ambalo linawahitaji wengi wa Benki hiyo.

Amesema Benki hiyo imeonesha utayari wa uwajibikaji kwa kuanza vyema Biashara na kuwataka kuingia katika ushindani wa kibiashara wa ubora wa Huduma wakizingatia PBZ ni Benki Kongwe Nchini.

 Nae Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt. Islam Seif Salum amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Wizara itasimamia Changamoto zote zinazoikabili Idara hiyo ikiwemo Ukosefu wa Magari  upungufu wa Wafanyabiashara na Changamoto nyengine.

Aidha ameutaka Uongozi wa Idara hiyo kuwasilisha Taarifa ya Mapendekezo ya Utatuzi wa Changamoto ambapo amewataka kuzingatia Mfumo wa Mtandao (E Office) katika kuandaa Miundombinu ya Ofisi.

Nae Mkurugenzi Uratibu wa Shughuli za SMZ Dodoma Ndg. Khalid Bakari Hamran ameeleza kuwa Ofisi ya Uratibu ina jukumu la kuratibu Shughuli zote za Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapokuwa Tanzania Bara pia kutoa huduma kwa Wazanzibari waliopo Tanzania Bara.

Nao Wakuu wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaofanyakazi zao Dodoma wamemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa Maamuzi ya kukutana nao kwa lengo la kujua namna wanavyofanyakazi ambapo wamemuhakikishia uwajibikaji mwema kwa kuendeleza Taasisi zao.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.