Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu Ikulu leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi Mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu anayefanyia Kazi zake Zanzibar (Konseli Mkuu).Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri, alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 21-11-2022, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi Mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu anayefanyia Kazi zake Zanzibar.(Konseli Mkuu) Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 21-11-2022.(Picha na Ikulu)   

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar, itaendeleza kasi katika kukuza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Saleh Ahmeid Alhemeir aliefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Alisema hatua ya nchi hiyo kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar kutatoa msukumo katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ilioanzishwa pamoja na ile inayolengwa kuanzishwa siku za usoni.

Alisema ni matarajio yake kuwa kupitia Konseli Mkuu Alhemeir, miradi mbali mbali inayotekelezwa na nchi hiyo kupitia taaisi na mashirika ya fedha ya nchi hiyo itafanikishwa.

Nae, Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu  hapa Zanzibar Saleh Ahmeid Alhemeir alisema hatua ya UEA kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar itaaongeza kasi ya mahirikiano na hivyo  akaahidi kufuatilia miradi mbali mbayo nchi hiyo imelenga ikisaidia Zanzibar.

Aidha, alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu ujenzi wa Ofisi za Ubalozi mdogo wa nchi hiyo hapa Zanzibar.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.