Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Bashungwa Ikulu Zanzibar

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.,Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, alipofika Ikulu Jijini Zanmzibar leo kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha. 11-11-2022


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Innocent Lugha Bashungwa (Mb) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 11-11-2022, mazungumzo hayo  yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Lugha Bashungwa  alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo  na kujitambulisha leo 11-11-2022, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.leo 11-11-2022

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kuanza kushughulikia migogoro ya Ardhi inayolikabili Jeshi la Wananchi na Tanzania, hapa Zanzibar.

Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Waziri wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa (MB) aliefika kwa ajili ya utambulisho.

Amesema kumekuwepo changamoto za migogoro ya ardhi inayolihusisha Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na raia, hali iliosababishwa na ongezeko la makaazi ya wa wananchi katika maeneo ya migogoro.

Dk. Mwinyi alisema amefurahishwa na juhudi zilizoanza kuchukuliwa na Wizara hiyo katika kuitafutia ufumbuzi migogoro hiyo, huku  akibainisha matumaini yake kuwa  itamalizika vyema.

Aidha, alimhakikishia Waziri huyo kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itampa kila aina ya  masharikiano ili kufanikisha majukumu ya kiulinzi.

Nae, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumkabidhi jukumu la kuiongoza Wizara hiyo, pamoja na kumshukuru Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kuweka misingi bora katika Wizara.

Waziri Bashungwa aliahidi kuendeleea kumsaidia Amiri Jeshi Mkuu katika ulinzi wa mipaka pamoja na kudumisha Muungano wa Tanzania.                                                             

Alisema Wizara yake iko mbioni kuitafutia ufumbuzi igogoro ya ardhi inayolikabili Jeshi la Wananchi wa Tanzania hapa Zanzibar.  

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.