Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari (Marine Spatial Planning - MSP) na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi katika Hotel ya Protea iliyopo mjini Dar es salaam, leo tarehe 28 Novemba 2022. Tanzania ni mwenyeji wa warsha hiyo inayohusisha wajumbe kutoka nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi.
Sehemu ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wanaoshiriki katika warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari (Marine Spatial Planning - MSP) na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi katika Hotel ya Protea iliyopo mjini Dar es salaam. Nchi zinazoshiriki ni pamoja na Tanzania, Komoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Re-Union na Afrika Kusini
Sehemu
ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wanaoshiriki katika warsha
ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari (Marine Spatial
Planning - MSP) na Ukanda wa
Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi katika Hotel ya Protea iliyopo mjini Dar
es salaam. Nchi zinazoshiriki ni pamoja na Tanzania, Komoro, Kenya, Somalia,
Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Re-Union na Afrika Kusini
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga leo amefungua warsha
ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu Mpango wa Matumizi ya Eneo la Bahari (Marine Spatial Planning - MSP) na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi katika Hotel ya
Protea iliyopo mjini Dar es salaam.
Amesema lengo la Warsha hiyo ni kujenga uwezo wa wataalamu kutoka nchi
wanachama wa Mkataba wa Nairobi katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Matumizi
ya eneo la Bahari, Usimamizi wa taarifa za Kimazingira, kubadilishana uzoefu na
kufahamu hatua zilizofikiwa na nchi wanachama katika kuandaa na kutekeleza mpango
wa Matumizi ya eneo la Bahari.
Bi. Maganga amesema Tanzania ni mwenyeji wa kikao kazi hicho
kinachohusisha wajumbe kutoka zaidi ya nchi 10 wanaotekeleza Mkataba wa Nairobi
unaohusu Hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa
Pwani ya Magharibi.
“Warsha hii imehusisha nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi na nchi zinazoshiriki
ni pamoja na Tanzania, Komoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji,
Shelisheli, Re-Union na Afrika Kusini “Alisisitiza Bi. Maganga.
Amesema warsha hii itasaidia kuja na mpango na usimamizi endelevu wa
matumizi ya rasilimali za bahari ikiwa ni pamoja na mgawanyo sahihi wa matumizi
ya bahari. Bi. Maganga amesema Tanzania inajipanga mapema katika kuandaa mpango
huo kwa kuzingatia kuwa uchumi wa bluu ni miongoni mwa agenda za dunia.
“Ninapozungumzia uchumi wa bluu ninasisitiza usimamizi endelevu na shirikishi
wa mifumo ikolojia ya Pwani na bahari ya Tanzania ili kuendelea kutoa bidhaa na
huduma muhimu ikiwa ni pamoja masuala ya uvuvi na uchimbaji wa mafuta na gesi
pale vitakakapogundulika”Alisisitiza Bi. Maganga
Warsha ya Mafunzo ya Kikanda kuhusu
Mpango wa Matumizi ya Eneo La Bahari (Marine Spatial Planning - MSP) Na Ukanda wa
Pwani Magharibi mwa Bahari ya Hindi na Kujenga Uwezo Katika Usimamizi wa Taarifa
za Mazingira imeanza leo tarehe 28 Novemba
na inatarajia kukamilika 1 Disemba 2022.
Warsha hii inafanyika katika Hotel ya Protea Jijini, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment