Habari za Punde

Waziri Mkuu aongoza waombolezaji kuaga miili ya wahanga wa ajali ya ndege ya Precision

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya watu waliopata ajali katika ndege ya shirika la Precision, iliyotokea Novemba 5, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za mwisho kwa miili ya watu waliopata ajali ya ndege  ya shirika la Precision  , iliyotokea Novemba 5, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za mwisho kwa miili ya watu waliopata ajali ya ndege  ya shirika la Precision  , iliyotokea Novemba 5, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole kwa ndugu wa Marehemu waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba yalipofanyika maombolezo ya kitaifa ya wahanga wa ajali ya ndege  ya shirika la Precision, Ajali hiyo ilitokea Novemba 5, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba - Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. 
Ndege ya Shirika la Precision  iliyopata ajali Novemba 6, 2022 ikiwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuvutwa kutoka eneo la ajali.
Miili ya marehemu waliofariki katika  ajali ya ndege  ya Shirika la Precision iliyotokea Novemba 5, 2022, ikiwa imewekwa katika eneo maalum kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera  kwa ajili ya kuagwa na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu katika maombolezo yaliyofanyika kweye uwaja huo  Jumatatu 7/11/2022. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza na kumfariji kijana Jackson Majaliwa kwa ushujaa wake wa kuwahi katika eneo ilipotokea ajali ya ndege  ya Shirika la Precision na kuwaokoa abiria waliokuwa wameshindwa kutoka ndani ya ndege hiyo. Maombolezo  ya kuaga miili ya watu wa ajali hiyo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera  7/11/2022.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.