Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Akielekea Dodoma Kuhudhuria Vikao vya Kikatiba vya CCM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Mkoani Dodoma kuhudhuria Vikao vya Kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Viongozi wa Serikali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Mkoani Dodoma kuhudhuria Vikao vya Kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemery Senyamule na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma, kwa ajili ya kuhudhuria Vikao vya Kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi-CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi,  akiambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi,  amewasili Dodoma jioni hii tayari  kuhudhuria vikao vya kikatiba vya Chama cha Mapinduzi na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utaofanyika tarehe 07/12  na tarehe 08/12.

 Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Dk. Mwinyi alilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wa mkoa wa Dodoma. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma, kwa ajili ya kuhudhuria Vikao vya Kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.