Habari za Punde

Serikali kutumia mifumo ya kisasa ukusanyaji mapato - Dk Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar kwa mwaka 2021/2022, Bodi ya Mapato Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 29-12-2022
                                             

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali imejipanga kutumia mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato ambayo itarahisisha kulipa kodi kwa wakati na kuongeza mapato ya nchi.

Alisema katika kufanikisha hatua hiyo, serikali imedhamiria kuibadilisha Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na kuwa Mamkala ya Mapato Zanzibar, (ZRA) ili kuenda sambamba na malengo ya serikali yaliyojiwekea katika kuwafikishia maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya shukurani na furaha kwa walipakodi Zanzibar, huko ukumbi wa Golden Tulipo, Uwanja wa ndege, Zanzibar leo Disemba 29, 2022.

Alisema lengo la kuundwa kwa Mamkala ya Mapato Zanzibar, siyo kupandisha kodi kwa walipa kodi, bali ni kutumia wigo mpana wa kuzidisha ukusanyaji wa mapato kwa njia za kisasa utakao kwenda sambamba na mifumo ya kiteknolojia ambayo itawarahishishia walipa kodi na sio kutumia nguvu kubwa kwa walipa kodi.

“lli Serikali ikusanye mapato zaidi mbali ya kuwa na Mamlaka  lakini kuwa karibu zaidi na walipakodi bila kutumia nguvu kwa walipa kodi wake, ili wafanyabiashara walipe kodi stahiki” alifafanua Rais Mwinyi.

Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashauri wananchi na wafanyabiashara kuendelea kujenga utamaduni wa kudai risiti wanapofanya manunuzi ya bidhaa ama huduma sambamba na kuwanasihi wafanyabiasha kutoa risiti mara baada ya kutoa huduma kwa wananchi.

“Kutokudai risiti wakati kwa kufanya manunuzi ni kuwanufaisha wachahce kwasababu kodi ikibaki kwa mfanyabiasahara itamnufaisha yeye na sio serikali” alifafanua Dk. Mwinyi.

Akiwazungumzia wanaohujumu mfumo wa ulipaji kodi, Dk. Mwinyi alitanabahishwa kwamba serikali haitosita kumchukua hatua Ofisa masuuli yeyote aliepewa jukumu la kuzuia mapato na kutokuyafikisha kwa wakati.

Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza Mamlaka ya Mapato ZRB kwa kuanzisha wazo la mwezi wa shukurani na furaha kwa walipakodi na kushauri kuwa wazo hilo liwe endelevu kila mwaka  ili kujenga uwelewa mpana na kutoa hamasa kwa wananchi kulipa kodi kwa wakati.

 Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Fedha  na Uchumi, Dk. Saada Mkuya alisema Mafaniko ya ukusanyaji wa mapato ZRB ni mafanikio yaliyofikiwa na kuboreshwa kwa mifumo mipya ya ukusanyaji kodi kwenye taasisi hiyo.

Alisema nia ya kuibadilisha Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na kuwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ilikuja baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kupitishwa muswada wa sheria  Disemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kuifanya Zanzibar kuwa na mapato yenye tija zaidi na kuifanya taasisi hiyo iwe na mtazamo chanya wa ukusanyaji wa mapato yake.

“Lazima utendaji ubadilike, ZRB iwe taasisi inayoaminika zaidi” alikazia Waziri Mkuya.

Nae Kamishna Mwenda wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Yussuf Juma Mwenda alisema ZBR ina lengo la kuongeza makusanyo ya kodi ili kufikia asilimia 100 ya makusanyo hadi mwezi Juni 2023 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo alieleza wanatarajia kukusanya shilingi milioni 579.

Anasema hadi mwezi Novemba mwaka huu ZRB ilifanikiwa kukusanya 238.5 bilioni na kueleza kuwa imefikia ufanisi wa asilimia 91 ya makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo ambayo kwa sasa alieleza imekua kwa asilimia 67.5

Alisema mafanikio hayo yanatokana na ufanisi wa ZRB chini ya usimamizi mzuri wa Waziri wa Fedha sambamba na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa kodi kwa ushirikiano mkubwa wa Serikali mtandao aliouelezea kwamba unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa mfumo huo utaanza kutumika rasmi mwezi Januari mwakani.

Aliongeza kuwa ZRB imeadhimisha siku ya shukurani walipakodi Zanzibar kutokana na ushirikiano mkubwa walioupata baina yao na kueleza kuwa katika kuifanikisha siku hiyo walifanikiwa kuwafuata walipa kodi na kusikiliza changamoto zinazowakabili za masuala ya ulipaji kodi na kuzitatua.

Alisema walifanikiwa kuwafikia walipakodi 442 pamoja na kuwatembelea wafanyabiasha 456 kwa lengo wa kuwasikiliza walipakodi hao na kuongeza kuwa ZRB ilifanikiwa kuzifikia kaya 100 kwenye kijiji cha Kangagani Pemba pamoja Kiojini Matemwe, mkoa wa Kaskazini Unguja kwa lengo la kuwapatia misaada ya kijamii sambamba na kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi na kudai risiti za kielektroniki.

Katika maadhimisho ya siku ya shukurani na furaha kwa walipa kodi Zanzibar kuliambatana na sherehe za ugawaji wa tunzo kwa walipa kodi waliochangia zaidi pato la taifa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo makundi manne muhimu yaliwania tunzo hizo wakiwemo Walipa kodi wakubwa kwa Unguja na Pemba ambapo jumla yao Kamisha Mwenda aliwataja ni 187 walifanikiwa kukusanyakodi zaidi ya asilimia 65 kwa Unguja na Pemba,  ikilinganishwa na walipa kodi wote, Kundi la walipa kodi kwa mikoa mitano ya Zanzibar ambao waligawiwa kwenye vipengele vya walipa kodi wanaowajibika, kwa kulipakodi kwa wakati, kutoa risiti  bila ya kusukumwa, kurejesha marejesho ya kodi kwa wakati na rikodi zao kwenye risiti zao hazipunguzi wala kuzidisha,

Aidha, kundi jengine lililopokea tunzo hizo ni Walipakodi wakubwa na Walipa kodi wanaotumia mfumo wa risiti za kielektoroniki. Zanzibar Petrtolium Ltd aliibuka mshindi wa Mlipakodi bora kwa mwaka wa Fedha, 2021/2022, ambapo tunzo yake ilipokelewa na Ndg. Altaf Jiwan mwakilishi mkaazi, Zanzibar.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.