Habari za Punde

SERIKALI KUWAPANGA UPYA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI NANYUMBU

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta Dkt Angeline Mabula akiwasili mkoani Mtwara na Mawaziri wenzake kwa ajili ya ziara ya siku moja ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 28 Desemba 2022.

Na Munir Shemweta, WANMM NANYUMBU                                                           

Serikali imeamua kuwapanga upya wananchi wa vijiji viwili vya Mbagala Mbuyuni na Marumba wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara ili kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi na kuleta usalama kwenye maeneo hayo.

 

Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Wanika kata ya Mkonona tarafa ya Nanyumbu wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara tarehe 28 Desemba 2022 wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta, Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, kitakachofanyika kila kijiji kitapewa utaratibu utakaosimamiwa na mkuu wa mkoa atakayewapanga wananchi wake na kuyaacha maeneo ambayo si salama kukaliwa na wananchi huku akisisitiza hakuna haki ya mtu itakayopotea.

 

"Mhe Rais anatambua tunayo shule yenye madarasa matatu, na hapa tulipo kuna kaya 94 ambazo ziko hapa na ukienda kitongoji jirani ziko kaya 134 hivyo serikali inajua idadi ya watu kwenye maeneo hayo na mahitaji yao" alisema Dkt Mabula.

 

Aliongeza kuwa, timu ya mawaziri nane wa wizara za kisekta inayozunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi sambamba na kuwafahamisha dhamira njema ya serikali yao katika kuhakikisha inalinda usalama wao pamoja na usalama wa mipaka ya nchi.

 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri nane wa wizara za kisekta, serikali itafuata utaratibu mzuri wa kuwapanga wananchi wa maeneo hayo kwenye vijiji husika ili kila mtu aweze kuendelea na maisha yake bila tatizo kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amejibu hoja ya changamoto iinayowafanya wananchi kuhama hama maeneo hayo.

 

"Kama mhe rais ametoa kinachostahili kipi ambacho kitakuwa kimebaki, ecolojia tunataka kuiona inavyokwenda ninyi wote ni mashahidi ukipita huo kina cha maji ki azidi kupungua kuna mahali unaona mchanga ni kwa sababu shughuli za kibinadamu zimeenda katika vyanzo vya maji" alisema Dkt Mabula.

 

Awali wananchi wa Nanyumbu waliieleza Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta kuwa, wao wamepokea maelezo na kusubiri kitakachofanyika.  Mkazi wa kitongoji cha Wanika Othman Said maarufu Gonga alibainisha kuwa, wao wanaishi kwenye vijiji hivyo kama nyumbani lakini pia kama walinzi na kueleza kuwa huko nyuma waliwahi kuwakamata watu waliodhaniwa kuwa ni alshabab.

 

Aidha, waliomba serikali kuchukua tahadhari wakati wa utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri na kushauri muda kuzingatiwa kwa kuwa hiki ni kipindi cha kilimo na watu wanaanza kwenda mashambani.

 

Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Mariamu Chaurembo aliwaambia wananchi wa wilaya yake kuwa, uamuzi wa serikali kupanga upya vijiji hivyo utatoa nafasi kwao kuanza kufanya shughuli za uchumi maeneo sahihi na kubainisha kuwa, vijiji vitatengenezewa matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kubainisha maeneo ya kilimo na ufugaji.

 

Awali akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mtwara Dkt Mabula alisema mkoa huo unahusisha migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji na mitaa 12 iliyoainishwa sehemu kuu tatu kulingana na aina ya mgogoro.

 

Aliitaja sehemu ya kwanza kuwa vijiji na mitaa 10 ambayo wananchi wake wataondolewa kwenye eneo la hifadhi na shamba la MATI na TARI huku sehemu ya pili ikihusisha kijiji kimoja ambacho mgogoro wake wa mipaka na hifadhi umerejewa kwa njia shirikishi kati ya halmashauri ya wilaya ya Masasi, Halmashauri ya kijiji cha Chingulungulu na Wataalamu wa Pori la Msanjesi lilipo chini ya TAWA.

 

Dkt Mabula alisema, sehemu ya tatu inahusu kuviondoa vitongoji 4 vilivyoingia hifadhi ya Msitu wa Mbagala na kuvimegea maeneo kutoka hifadhini karibu na vijiji mama huku sehemu ya nne ikihusisha kumega eneo la hifadhi ya Ndechela na kuwaoa wananchi wa kijjji cha Nakopi ambapo halmashauri ya Nanyumbu kwa kushirikiana na TFS pamoja na serikali ya kijjji wamelitekeleza.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.