Habari za Punde

WUSM Wakabidhi Gari

Na.Adeladius Makwega- Mji wa Serikali.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini ndugu Abel Philip amekabidhi gari aina ya Toyota Coaster lenye namba ya usajili STM 2639 kwa MkurugenzI Msaidizi wa Utawala na Rasimali Watu Bi Zahara Guga Desemba 27, 2022 Jijini Dodoma kwa shughuli kadhaa za utendaji.

Akizunguma katika makabidhiano hayo Kaimu Katibu Mkuu huyu ambaye pia Kaimu Mkurugenzi anayesimamia Idara ya Sera na Mipango wizarani hapa amesema kuwa gari hiyo iliyonunuliwa kwa shilingi 236, 213, 589.29/- itatumika katika kuboresha utendaji kazi wa wizara hii na kuwafikia wadau wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.

“Ninakabidhi chombo hiki kikiwa imara na ubora wake, matarajio ya serikali Idara ya Utawala na Rasilimali watu itahakikisha gari hili linatunzwa na wanaoliendesha na wanaolipanda kwa nyakati tofauti, litumike ipasavyo katika kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa ili tukamilisha malengo ya ununuzi wake na kutunza mali za umma.”

Akizungumza mara baada ya kulipokea basi hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bi Zahara Guga amemuhakikishia Kaimu Katibu Mkuu kuwa gari hilo litatunzwa vizuri kama ilivyokusudiwa.

“Tayari Afisa Usafirishaji ameshampangia dareva wa kuliendesha yu tayari kwa kuanza kutoa huduma kwa watumishi na wadau katika shughuli kadhaa za wizara yetu.”

Basi hii yenye matairi 6, injini ya 1 HZ, spidi mita ni 160 lina uwezo wa kubeba abiria 30 kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.