Habari za Punde

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ni mdau muhimu wa sekta ya maendeleo Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel Tutuba (kulia kwa Rais) akiwa na Gavana Mstaafu wa (BOT)  Prof Florens Luoga , alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 18-1-2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ni mdau muhimu wa sekta ya maendeleo Zanzibar pia ni mshauri mzuri kwa masuala ya uchumi wa nchi.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipokutana na Gavana mpya wa benki Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw.Emmanuel Mpawe Tutuba, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha tokea alipoteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Januari 07 mwaka huu.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekua na ushirikiano mzuri na BOT wakati wote pamoja na kupata ushauri mzuri wa uendeshaji wa uchumi wa Zanzibar.

Aliongeza Zanzibar imepata mafanikio makubwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania nakueleza ushirikiano wa taasisi mbili hizo umejenga ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao ipasavyo.

Aidha, Rais Mwinyi alimuahidi Gavana huyo kushirikiana nae kwenye majukumu yake kwa kipindi chote cha uongozi wake  na kumshauri kuendeleza alipofikia mtangulizi wake.

“Nikupeahadi tuu ya ushirikiano wetu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tukiwa wadau Muhimu wa kazi zinazofanywa na  Banki Kuu, tupo tayari kushirikiana vya kutosha kwa masuala yote yanayohitaji ushirikiano wetu” aliahidi Dk. Mwinyi.

Alimuahidi Gavana huyo kufanyanaye kazi bega kwa begwa kwa msaada mkubwa wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisi zake, na kuongeza kwamba kazi nzuri ilifanywa na mtangulizi wake ilileta mafanikio makubwa kwa Serikali.

Akizungumzia changamoto za uchumi wa dunia, Dk. Mwinyi aliweleza Gavana Tutuba kwamba washirikiane kutafuta ufumbuzi mzuri wa kuzigeuza changamoto hizo kuwa fursa ili zilete tija kwa taifa pamoja na kuziangalia kwa kuzizibiti ili zisiathiri uchumi wa nchi.

Rais Mwinyi alimuahidi Gavana huyo kushirikiana nae kwenye majukumu yake kwa kipindi chote cha uongozi wake  na kumshauri kuendeleza alipofikia mtangulizi wake.

Alimuahidi Gavana huyo kufanya naye kazi bega kwa  msaada mkubwa wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisi zake, na kuongeza kwamba kazi nzuri ilifanywa na mtangulizi wake ilileta mafanikio makubwa kwa Serikali.

Hata hivyo, Dk. Mwinyi alimshuru Gavana aliemaliza muda wake, Prof. Florens Luoga kwa ushirikiano wake alioutoa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kipindi chote cha utumishi wake kwa Taifa, nakueleza kwamba wakati mwengine hakuishia tuu kwenye ngazi ya wizara bali alifika hadi ngazi za juu katika kufanikisha majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu.

Naye, Gavana Tutuba alisema Banki Kuu ya Tanzania ni chombo cha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kinachofanya kazi zake kwa pande zote mbili za Muungano katika kusimamia masuala ya kiuchumi na sera za fedha kwa Zanzibar na Bara.

Alisema serikali zote mbili zipo kwaajili ya kulinda maslahi ya wananchi kwa kudhibiti mfumko wa bei duniani uliochangiwa na athari kubwa za kupanda kwa bei za mafuta ambayo inaathiri zaidi sekta ya usafirishaji kwa wananchi.

Alitumia fursa hiyo kuzipongeza serikali za SMZ na SMT kwa kuendelea kuwasaidia wananchi wake kuwapunguzia makali yanayotokana na athari hizo

Kwa upande wake, Gavana wa zamani, Prof. Florens Luoga alitumia fursa hiyo kumuaga Rais Dk. Mwinyi baada ya kumaliza muda wa utumishi wake kwa Benki kuu ya Tanzania pia Prof. Luoga alimshukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano iliyoutoa kwake muda wote wa utumishi wake.

NA MWASHAMBA JUMA, IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.