Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 11-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Juma (kulia kwa Rais) na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu leo 11-2-2023 na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalum na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Juma na Ujumbe wake baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-2-2023.(Picha na Ikulu)
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi azitaka mahakama kuu ya Tanzania na Zanzibar kutengeneza mfumo endelevu wakuboresha mageuzi ya kiutendaji yaliyofanyika kwa lengo la kudumisha juhudi za mahakama hizo kuwa endelevu katika kuwatumikia watu.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Majaji na watendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar.

Alisifu ushirikiano  wa kiutendaji uliopo baina ya Mahakama hizo baada ya mabadiliko makubwa waliyoyafanya baina yao ambayo alieleza yameongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao, pia alizishauri taasisi mbili hizo za sheria kuendeleza ushirikiano wao katika kufanikisha malengo yao.

“Nataka niseme, kama kuna sekta katika Muungano wetu zenye ushirikiano wa karibu ni Mahakama kuliko sekta nyengine na nawashukuru Mahakama Kuu Zanzibar kwa kulichukulia hilo kwa uzito wake, wamenitaarifu kwamba wako kwenye mabadiko makubwa ya kubadili ufanisi wa utendaji wao” Alisifu Dk. Mwinyi.

Alimuagiza Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kufuata mfumo wa Mahakama kuu ya Tanzaia kwa sehemu kubwa ya mabadiliko iliyoyafanya kwenye utendaji wao ili na Zanzibar ipige hatua kubwa kiutendaji kama walivyofanikiwa Tanzania Bara.

Alisema, Zanzibar ina mengi ya kujifunza kwa Mahakama Kuu ya Tanzania, hivyo aliwataka watendaji wa Mahakama kuu Zanzibar kujitahidi kuisarifu teknolojia ili kuendana sambamba na mifumo yakisasa iliyopo katika kuwawepesishia kazi zao ili wananchi wapate huduma kwa haraka zaidi kwa lengo la kurejesha imani zao kwa mahakama.

Akizungumzia thamani ya mahakama kwenye ukuaji uchumi wa nchi, Dk. Mwinyi alieleza ukuaji uchumi unategemeana na mihimili yote ya Serikali kufanyakazi kwa usirikiano na alieleza mabadiko makubwa yakiufanisi yaliyofanywa kwenye mahakama hizo anaamini yatarejesha hadhi ya utendaji na kuitaka mihimili mengine ya Serikali kufanya mabadikilo kama walivyofanikiwa Mahakama ili kurejesha imani za Wananchi.

“Ikifika sehemu wananchi wakaanza kusema hatuna imani na mahakama anajua akienda mahakamani atachukua muda mwingi kupata haki yake, au uwezo wa kulipia hadi apate haki yake hana, basi ile kukata tamaa tuu inatufanya kama serikali lazima tuone jinsi gani hii Mihimili inasaidia watu kurejesha imani zao” Alisihi Dk. Mwinyi.

Rais Dk. Mwinyi, aliishukuru Mahakama Kuu Tanzania kwa msaada wao wakujenga kituo jumuishi Pemba na kueleza kwamba juhudi hiyo ni msaada mkubwa kwa Serikali.

“Nishukuru sana kwa utayari wenu wa kusaidia Serikali kujenga kituo hiki jumuishi Pemba,  ni dhamira njema kwa nchi yenu, tunashukuru sana na hayo yaliyobaki tutayafanyia kazi sisi wenyewe” alishukuru DK. Mwinyi.

Naye, Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alisema Mahakama imejipanga vizuri kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa haki yake licha ya ukubwa wa nchi na wingi wa watu wake, mgawanyiko wa idadi ya mikoa yake, wilaya, vijiji na vitongoji kila mmoja mahakama imelenda kumfikia, hivyo alieleza lazima mahakama zijipange hukakikisha zinawafika watu wote na kila mmoja anapatiwa haki yake.

Alisema Mahakama ya Tanzania imefanikiwa sana kutokanana maboresho yake ambayo yalianza mara tuu baada ya nchi kupata uhuru wake.

Alisema maboresho zaidi ambayo Mahakama imekuwa ikiyafanyia kazi ni yale yaliyofanywa na Tume ya Jaji Bomani mwaka 1993 ambapo Mahakama imeangalia matatizo nane na imeanza kuyatekeleza kwa vitendo.

Alieleza matatizo hayo ni ucheleweshwaji wa kutatua migogoro inayofikishwa mahakamani ambayo alieleza yanaendelea kufanyikwa kazi kwa kutumia mifumo wa kisasa ya kiteknolojia.

Alieleza eneo jengine ni wananchi kuwa na fursa ya kupata haki zao kwa kwenda kwenye majengo ya mahakama kufuata taratibu za kisheria na kupata taaluma juu ya haki zao. Aidha kudhibiti rushwa na utovu wa maadili kwenye mahakma jambo alilolieleza bado ni vita endelevu, tatizo jengine walilojielekeza ni sheria kutokua na uharaka wa kutoa maamuzi kwa vile ni za zamani kwahiyo, alieleza mahakama sasa zinafanya mabadiliko makubwa kwenye eneo hilo kwa msada wa teknolojia, aidha, kurejesha imani ya wananchi kwenye vyombo vya sheria katika kuwapatia haki zao.

Eneo jengine wanaloliangalia alieleza ni uwezo wa majaji, mahakimu na mawakili kulingana na taaluma zao pamoja na uchache wa watoa kuduma kulingana na mahitaji ya wananchi, Jaji Ibrahim alisema  pamoja na miundombinu ya majengo ya mahakama  lakini zaidi kwenye kupata huduma bora.

“Sisi mahakama baada ya kuona matatizo kwenye vituo vya sheria ni makubwa sana, tumekua tukitegemea zaidi wizara ya Katiba na sheria ziongoze, tumeona bora tubadili mwelekeleo, sasa sisi Mahakama ndio tuwe kiini cha maboresho hayo” alifafanua Jaji Ibrahim.

Nae, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, aliishukuru Mahakama Ya Taznaznia kwa ushirikiano inayoendeelea kutoka kwa Mahakama ya kuu ya Zanzibar tokea alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Pia aliahidi kwenda sambamba na kasi ya Mahama ili kuleta mabadiliko makubwa Zanzibar.

Akizungumza kwenye ghafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole gabriel  alieleza sehemu kubwa ya maboresho iliyofanya mahakama hiyo ni matumizi ya mifumo kwa majengo yote kuunganishwa na mtandao na utendaji mzima wa Mahakama, ikiwemo matumizi ya tehama na teknolojia ya kisasa katika uendeshaji kesi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kitelektroniki na na kidijitali.

Aliongeza mifumo hiyo imeweka miundombinu yote ya mahama kwa kuweka kipaumbele cha matumizi ya teknolojia wakati wa kusikiliza kesi hali iliyorahisisha kesi nyingi kusikilizwa kwa wakati mfupi, matumnizi ya mifumo ya simu imeleta mabadiliko makubwa.

Alieleza matumizi ya mifumo hiyo imeongaza ufanisi kwa utendaji wa makakama ambayo imerahisisha kazi, pia alisema teknolojia imesaidia kuziunganisha mahakama zote Tanzania kwenye mfumo mmoja wa kidijitali ambao umerahisisha utendaji wao kutoka mahakama ya mwanzo hadi Mahakama kuu.

Alisema katika kurahisisha utendaji wao mifumo imefanikiwa kuunganisha Mahakama na wadau wengine wote wa taasisi za Mahakama ili kuwepesisha kazi na kuokoa muda wa kuendashaji wa kwa kutumia teknolojia hiyo.

Alisema mifimo pia imezisaidia mahakama kupata taarifa nyingi zaidi wakati wakusikiliza mashauri, kutokana na ushikiano baina ya mahakama na taasisi zake.

Hata hivyo, alieleza mifumo hiyo pia imechangia kuanzisha kituo cha kuratibu, kusimamia na kufuatilia mwenendo wa mahakama zote Tanzania kwa njia ya mtandao kwa kusaidiwa na wataaalmu wa ndani ambao hudhibiti hitilafu wakati mahakama zikiendelea jambo alilolieleza kwamba wataalamu hao wanauwezo wa kuimiliki wenyewe na kuisawazisha wakati wa hitilafu.

Ujio wa ugeni huo unakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.