Habari za Punde

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AONGOZA KAMATI YA UANGALIZI YA SADC NCHINI LESOTHO

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius Mhe. Paramasivum Pillay Vyapoory Pamoja na Ujumbe wa Seneti ya Lesoth alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.


Na Mwandishi Maalumu

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye 

pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika 

(SADC Panelof Elders, POE) ameongoza Ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC

inayofuatilia Utekelezaji wa Makubaliano ya Amani nchini Lesotho katika ziara nchini 

humo tarehe 08 – 11 Februari 2023.

 

Ziara ya Kamati hiyo ya Uangalizi ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Wakuu wa Nchi na

Serikali wa SADC katika Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika

Kinshasha, DRC mwezi Agosti 2022 ambapo walilielekeza Baraza hilo la Wazee la SADC

kufuatilia kwa karibu jitihada za usuluhishi wa migogoro inayoendelea kwa muda mrefu

katika Falme za Lesotho na Eswatini.

 

Rais Mstaafu Kikwete ameongozana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius,

Paramasivum Vyapoory, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wazee 

amepata wasaa wa kukutana na Mtukufu Motlotlehi Letsie III, Mfalme wa Lesotho, 

viongozi wakuu wa Serikali ya Lesotho pamoja na wadau wengine muhimu katika mgogoro huo.

 

Kamati pia imepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lesotho

ambaye ndiye Mkuu wa Serikali, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Haki, Sheria na

Masuala ya Bunge, Spika wa Bunge, Makamu Rais wa Seneti, Waziri wa Mambo ya Nje na

Uhusiano wa Kimataifa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiongozi wa Tume ya Taifa ya

Mabadiliko, Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyo Bungeni, Vyama vya Siasa

vilivyo nje ya Bunge, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Askofu Mkuu wa Baraza la Kanisa la

Kikristu nchini Lesotho pamoja na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza, 

AfrikaKusini na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa.

 

Katika mikutano yote iliyofanyika, Kamati hiyo imesikiliza kwa kina maoni ya wadau hao

wote kuhusu namna bora zaidi ya kuweza kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari

imeshafanyika katika kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro uliopo nchini humo. Kamati hiyo

inaripoti kwa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya

Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) ambaye kwa sasa ni Hage Geingob,

Rais wa Namibia.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius Mhe. Paramasivum Pillay Vyapoory Pamoja na Ujumbe wa Seneti ya Lesoth alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana  viongozi wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Lesotho alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na kikao na Mwanasheria Mkuu wa Lesotho Mhe. Rapelang Motsieloa alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.