Amina Massod kutoka Redio jamii mkoani Pemba alieibuka kuwa mshindi wa kipengele cha redio jamii.
Zuhura Juma Saidi kutoka mtandao wa Pembaportal alieibuka mshindi wa tuzo ya wanahabari kupitia mtandao wa kijamii akikabidhiwa zawadi na katibu mtendaji wa Tume ya utangazaji Zanzibar Suleiman Abdalla.
·
Radio jamii na mitandao
ya kijamii zang’ara
Jumla
ya waandishi wa habari 10 wameibuka kidedea katika tuzo za umahiri za uandishi
wa habari za takwimu za wanawake na uongozi zilizoandaliwa na TAMWA, Zanzibar
kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya
ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO).
Miongoni
mwa vipengele ambavyo vilikuwa vinashindaniwa ni pamoja na mwandishi mahiri
katika kipengele cha radio za kitaifa, radio za kijamii, magazeti pamoja na
mitandao ya kijamii, ambapo kwa upande wa magazeti kulikuwa na washindi watatu,
mitandao ya kijamii watatu, radio za kijamii washindi wawili na washindi wawili
kutoka katika radio za kitaifa.
Katika
washindi hao 10 waliopatikana, jumla ya washindi wane (4) wa kwanza kutoka
katika kila kipengele walipatiwa zawadi na cheki ya milioni moja, tuzo pamoja na vyeti vya
ushiriki.
Washindi
hao wanne kutoka katika kila kipengele ni pamoja na Husna Mohammed Khamis
kutoka gazeti la Zanzibar Leo, Rehema Juma Mema kutoka radio Asalaam FM, Zuhura
Juma Said wa mtandao ya kijamii wa Habari Portal na Amina Masoud Jabir kutoka
radio Jamiii Mkoani kisiwani Pemba, ambapo washindi wa pili nao walijipatia
vyeti pamoja na cheki ya shilingi laki tano (5) kwa kila mmoja, ambapo mshindi
wa tatu katika kila kipengelke alizawadiwa cheti pamoja na cheki ya shilingi
laki nne (4).
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajauni,
Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt
Hussein Ali Mwinyi ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana
na Michezo, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita alisema kuwa kilio cha wanahabari
kuhusu mabadiliko ya sheria ya huduma ya habari kuwa Serikali imewasikia na ipo
njiani kuzibadilisha ili muifanye kazi yenu kwa umahiri zaidi na bila ya
wasiwasi wowote.
“Tunataka
kuwa na sheria ambayo imetokana na pande mbili yaani wadau wa habari na
Serikali”, amesisitiza Waziri Tabia.
“Nimekuwa
nikifuatilia vyombo vya habari na kuona kuwa
Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya
mwaka 1988 na marekebisho yake ya mwaka 1997 na
Sheria No.8 ya 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2010 zikilalamikiwa
zaidi kuwa na mapungufu na zinahitaji kurekebishwa pamoja na sheria nyingine kadhaa zinazohusiana nazo” alisisitiza.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Zanzibar Dkt.Mzuri Issa aliiomba
Serikali kuhakikisha kwamba ile asilimia 40 ya ushiriki wa wanawake inafikiwa
katika kila nyanja ya vyombo vya maamuzi ikiwemo kamati, bodi za utendaji, hivyo
hakuna budi kuwa na mazingira mazuri ya kuwewezesha wanawake kushiriki katika
uongozi katika ngazi zote.
“Tunasisitiza
pia kuandaa takwimu za wanawake na Uongozi jambo hilo litasaidia kujua hasa
tuko wapi katika malengo hayo ambayo ni ya kimilenia, lengo nambari 5 la
milenia (sustainable development goal, SDG), na sisi taasisi zetu tunaahidi
kutoa mashirikiano ya kina”. Aliongeza Dkt Mzuri Issa.
Tuzo
hizi za uandishi wa habari za takwimu kwa wanawake na uongozi ni muhimu sana
katika kushajihisha waandishi wa habari wa Zanzibar kuandika zaidi habari na
makala kuhusiana na masuala ya wanawake na uongozi, lakini pia kutoa takwimu ya
idadi sahihi ya wanawake walioko katika uongozi Zanzibar.
TAMWA,
Zanzibar imeamua kuchukua juhudi mahasusi za kuandaa tuzo hizo ili jamii
itambue mchango wa wanawake na uongozi katika sekta mbalimbali ili kuinua hali
za wanawake na kuongeza ushiriki wao
katika masuala ya uongozi ili kufikia 50 kwa 50 katika katika ngazi zote
za maamuzi kama inavyoelezwa katika katiba nchi yetu na mikataba na itifaki
mbali mbali za kimataifa.
TAMWA,
Zanzibar inatoa wito kwa waandishi wa habari wa zanzibar kuendelea kuandika
habari zinazohusu wanawake, takwimu lakini pia vikwazo mbalimbali vinavyomzuia
asifikie nafasi za uongozi na kuwa tayari kushiriki katika tuzo zijazo ambazo
zitaandaliwa.
Tuzo
hizo ambazo ni mara ya pili kutolewa zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kwa kushirikiana na Jumuiya ya
Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na
Utetezi Pemba (PEGAO) na Ubalozi wa Norway.
Jumla
ya kazi 421 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio, televisheni
pamoja mitandao ya kijamii, zilipitiwa katika kutafuta washindi hao katika tuzo hizo zenye kauli mbiu “KALAMU YANGU
MCHANGO WANGU KWA WANAWAKE” hivyo waandaji wa tuzo hizo zinawaomba waandishi wa
habari kujitahidi kuandika habari za kina za wanawake na uongozi.
Dkt. Mzuri Issa
Mkurugenzi
TAMWA, ZNZ.
No comments:
Post a Comment