Habari za Punde

Wanaume na Wavulana wamehimizwa kushiriki kikamilifu kupinga Mila na Desturi zenye madhara ili kutokomeza ukeketaji.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt. Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake yanayotarajiwa kufanyika  Februari 06 hufanyika kila Mwaka.

Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum ameyasema hayo jijini Dodoma alipozungumza na Waandishi wa Habari kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake yanayofanyika  Februari 06 ya  kila Mwaka.

Mhe. Gwajima amesema  maadhimisho hayo yanlenga kutokomeza vitendo vya ukeketaji dhidi ya Wanawake na  kaulimbiu ya Mwaka huu ni 
“Wanaume na Wavulana; Tushiriki Kupinga Mila na Desturi zenye Madhara ili kutokomeza Ukeketaji”. 

Amesema kaulimbiu hiyo inatambua umuhimu wa wanaume katika kushawishi Wanawake na watoto wa kike kutowafanyiwa ukeketeaji.

"Wanaume inatakiwa kubadilika kwanza ndipo jitihada za kupinga ukeketaji zinaweza kufanikiwa.
Takwimu zinaonyesha kuwa ukeketaji nchini bado ni tatizo hali inayotokana na baadhi ya Jamii zetu kuendelea kukumbatia mila na Destpuri zenye madhara na Kuwadhalilisha watoto wa kike.” alisema Dkt Gwajima.

Dkt Gwajima amesema Serikali inaendelea na jitihada za kukabiliana na vitendo Vya ukeketaji kupitia mipango na Mikakati iliyowekwa ikiwemo kutunga na kufanya marekebisho .

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1997) inasisitiza  usawa  na heshima kwa binadamu wote, Kutambua na kutathmini utu wa Mtu Pamoja na Kuhakikisha haki mbele ya Sheria”  

Aidha ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika ngazi zote kwa kuandaa Mdahalo wa Wadau wanaotekeleza shughuli za kutokomeza ukeketaji nchini pia kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukeketaji kwa njia ya mikutano ya hadhara, vikao na maandamano. 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Asha Vuai amesema Serikali inaendelea  na juhudi za kupinga ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto hasa katika mikoa iliyoathiriwa na ukatili huo akitaja mikoa inayoongoza nchini.

“Mkoa Mikoa inayoongoza kwa ukeketaji ni Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%) Singida (31%) Tanga (14%), Iringa (8%), Njombe (7%), na Pwani (4%)" amesema Aisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.