Habari za Punde

DKT. Tax Amekutana kwa Kuzungumzo na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Uingereza na Tanzania na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha na kuendeleza uhusiano huo.

Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.