Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania leo tarehe 31 Machi 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango akimuaga Makamu wa Rais wa Marekani
Kamala Harris na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha
ziara nchini Tanzania.
(Picha Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment