Habari za Punde

Dua ya Kuwaombea Viongozi wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Inaendelea Kufanyika Zanzibar

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed(mwenye kofia nyeupe na koti)akijumuika pamoja na wanafamilia na wananchi mbalimbali  katika Dua ya kumuombea aliekua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Almarhumu Khamis Darweshi Mdingo,katika maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa kwanza wa Chama cha Afroshirazi na Siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed  akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa ya Serikali   katika Dua ya kuwaombea aliekua Kanali Mstaafu  Almarhumu Seif Bakari Omar,na Aliekua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Almarhumu Khamis Darweshi Mdingo .katika maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa kwanza wa Chama cha Afroshirazi na Siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed akizungumza na akina mama Ndugu wa Marehemu Khamis Darweshi Mdingo na Marehemu Seif Bakari Omar baada ya kumaliza Dua ya kuwaombea Marehemu hao katika  maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa kwanza wa Chama cha Afroshirazi na Siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.02-04-2023.


Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar. 

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mheshimiwa, Dkt.Khalid Salum Mohamed amesema katika kuwaenzi viongozi wa kitaifa ipo haja ya kuandikwa historia zao ili vizazi viweze kupata kumbukumbu sahihi za viongozi hao.

 Hayo ameyasema huko Kiembe Samaki, Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja wakati wa  kufanya ziara na kusoma dua katika kaburi la Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Jeshi la Polisi Marehemu Khamis Darwesh Mdingo na  Kaburi la Kanal Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omar .

Amesema kila nchi ina utaratibu wake wa kuwaenzi viongozi wake kutokana na sababu zake, kwani wao ndio chimbuko la Mapinduzi ya  mwaka 1964 ambayo yalileta uhuru, usawa pamoja na maendeleo ya kijamii na kiuchumi ambayo matunda yake yanaonekana hadi sasa  .

 Aidha alisema kuwa  viongozi hao wa kitaifa walifanya mengi katika nchi hii  kutokana na  jasho lao ikiwemo kuunganisha Nchi mbili kati ya Tanganyika na Zanzibar na kupata muungano wa Tanzania  .

Alifahamisha kuwa Serikali imeandaa utaratibu wa kisheria wa kuwaenzi viongozi wa kitaifa katika sheria ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2021 iliyoweka utaratibu ya wiki wa kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi

 Nae Msemaji  wa Familia Jafar Abdalla Mussa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia hiyo  kwa kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ujio huo wa kufanya ziara ya kusoma dua kwa Marehemu wazee wao .

Aidha ameiyomba  Serikali kuwa karibu na vizazi vya marehemu hao ili kupata msaada mbali mbali unapohitajika katika familia hiyo .

Ibada ya kuwaombea dua Marehemu Khamis Darwesh Mdingo na Marehemu Seif Bakar Omar imeongozwa na Kadhi wa Wilaya Sheikh Hemed Saleh Ali .

Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaezi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi  na Siku ya  Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume hufanyika kila mwaka katika wiki ya mwanzo wa mwezi wa nne

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.