MAKAMU Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kukijenga chama kiuchumi kwa kuimarisha
miundombinu wezeshi ya utendaji kwa watendaji wake ili kuboresha ufanisi ndani
ya chama hicho.
Rais Dk. Mwinyi
aliyasema hayo alipozungumza kwa mara ya kwanza na viongozi wa chama cha
Mapinduzi (CCM) ngazi ya mashina, majimbo, wilaya, hadi Mkoa, kwenye ukumbi wa
Piccadilly, uliopo Kombeni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu Mwenyekiti
huyo alieleza ili chama kifanye kazi zake kwa ufanisi ni lazima kiwe na vifaa
vya kutendendea kazi vikiwemo vyombo vya usafiri na vifaa vya kisasa vya
ofisini vyenye hadhi na umri wa chama hicho.
“Tutafanya kila
linalowezekana kukijenga chama kiuchumi” alieleza Mamamu mwenye kiti huyo.
Aidha, Rais Dk.
Mwinyi alikiahidi chama kukitendea makubwa zaidi wakati huu wa uongozi wake
ikiwemo kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano ambao chama utajivunia nchi nzima na
kueleza maendeleo makubwa yaliyofikiwa Zanzibar ni utekelezaji wa Ilani ya
chama ambayo kwasasa imefikia nusu ya utekelezaji wa ahadi zake na kwamba
sehemu ndogo iliyobaki itakamilishwa kwa wakati.
Alisema, CCM ina rasilimali nyingi nakueleza baadhi ya rasilimali hizo
hata bado hazijatendewa haki.
Akizungumzia suala la
umoja na mshikamo ndani ya Chama hicho, Makamu Mwenyekiti huyo, alionya
mfarakano na mgawanyiko ndani ya Chama na kuwaasa wanachama wawe kitu kimoja
ili kuongeza nguvu ya chama chao.
Alisema wakati wa
chaguzi zote huibuka makundi mbalimbali yenye dhamira na maslahi tofauti hivyo,
aliwaasa wana CCM kurejesha umoja na mshikamano mara baada ya uchaguzi
kukamililka.
Aidha, alionya endapo
ikitokea hali ya mgawanyiko wa makundi ndani ya chama hicho, ameziagiza kamati
za maadili kuchukua hatua kali za nidhamu na kuhakikisha nidhamu na mshikamano
ndani ya chama unarejea.
Akizungumzia suala la
uhai wa chama, Makamu Mwenyeki CCM, Rais Dk. Mwinyi, aliwataka viongozi wenye
dhamana kwa mujibu wa nafasi zao ndani ya chama hicho, kutekekeza jukumu na
kuongeza wanachama wepya ili kuendelea kukipa uhai chama hicho kiendee kushika
dola.
“Mtaji wa chama chetu
ni kuongezeka wanachama wepya, kadi ziwepo za kutosha” alisisitiza Makamu
Mwenyekiti huyo.
Vilevile, Rais Dk.
Mwinyi aliwahimiza wana CCM kulipa michango kwa wakati badala ya kusubiri hadi
vipindi vya uchaguzi vikaribie.
Katika hatua
nyengine, Rais Dk. Mwinyi, aliagiza chama kuwapa mafunzo ya uongozi watendaji
wa ngazi zote walioshinda kwenye uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana
pamoja na kujipanga tena kwaajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Naibu Katibu mkuu
CCM, Zanzibar Dk. Muhamed Said Muhamed Dimwa,
akizungumza kwenye hafla hiyo, alieleza CCM haitajibu maneno
wanayorushiwa na wapinzani badala yake wataendelea kuitekeleza Ilani ya chama
chao kwa kuboresha maendeleo ya nchi na watu wake na kuahidi kutowafumbia macho
wenye dhamira ya kukwamisha ilani ya chama hicho.
Nae, Mjumbe wa Kamati
ya siasa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa
aliwaasa wanachama wa CCM kuwachagua viongozi wenye sifa na weledi wa
kuwatumikia sio kuwanunua viongozi wakati wa chaguzi za chama hicho, pia
alieleza kuna ushirikiano wa moja kwa moja baina ya chama na Serikali katika
kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Kwa upande wake,
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake, Tanzania Zainab Khamis Shomari,
alieleza ahadi ya wanawake na kinamama Tanzania bado ipo palepale ya kurejesha
ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
Pia aliishukuru
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwajengea heshima wanawake kwa
kuwapa fursa ya uongozi kwenye sekta mbalimbali.
Naye, Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Magharibi Kichama, Muhamed Rajab Soud, alishukuru Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuufungua kimaendeleo mkoa huo kwa kuwepo
na wawekezaji mbalimbali jambo alilolisifu wamewajengea heshima kubwa kwenye
Mkoa wao.
Huo, ulikua mkutano
wa kwanza wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Mwinyi na
viongozi wa chama hicho kwa ngazi za mashina, majimbo, wilaya, hadi Mkoa, tokea
kumalizika wa chaguzi za chama hicho, mwishoni mwa mwaka jana.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU - ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment