Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Uongozi wa Taasisi ya Qatar Foundation

 

Mke wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi, amekutana Mhe. Sheikha Moza bint Nasser, ambaye ni mama ya mfalme wa Qatar Tamir bin Hamad Al Thani ambaye pia ni muasisi na mwenyekiti wa Qatar Foundation. 

Mama Mariam Mwinyi alipata fursa ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya kuimarisha jitihada mbalimbali za kuwainua kiustawi, kielimu na afya  za wanawake, vijana na watoto.

Wakiwa katika mkutano huo Mhe. Sheikha Moza ameonyesha nia ya awali ya kushirikiana na Mama Mariam Mwinyi kupitia ZMBF katika kuimarisha mikakati ya kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, vijana na watoto  Zanzibar. 

Aidha Mama Mariam amempongeza pia Mhe. Sheikha Moza kwa kujitolea kuwekeza katika sekta ya Elimu na Afya nchini Qatar na sehemu mbalimbali duniani na baadae kumkaribisha pia Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.