Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na Mjane wa Marehemu Malim Seif Sharif Hamad Mama Awena Sinani Masoud wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Garagara wilaya ya Magharib "A" leo tarehe 28.05.03. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza na wananchama na wafuasi wa chama hicho waliofika kumsikiliza katika viwanja vya Garagara Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja
Wafuasi wa Chama cha ACT -Wazalendo Zanzibar wakiwa katika Mkutano wa hadhara wa chama hichoi uliyofanyika katika viwanja vya Garagara Wilaya ya Magharib A Unguja wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Othman Masoud Othman alipokuwa akihutubia wanachama hao katika mkutano huo.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka wazanzibari kujipangana kushiriki ipasavyo katika mchakato wa katiba muda utakapowadia ili kuweza kuyasema vyema masuala mbali mbali kwa maslahi ya Zanzibar.
Mhe. Othman ameyasema
hayo huko katika Viwanja vya Garagara wilaya ya Mgharibi ‘A’ Unguja alipozungunza
katika Mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioelezea juu ya masuala mbali mbali
yanayohusu maendeleo ya Zanzibar.
Amesema kwamba wananchi
ni lazima watimize wajibu wao huo katika kuhakikisha wote wanashiriki
kikamilifu kwenye mchakato huo wa katiba kwa kuwa hakuna mtetezi wa maslahi ya
Zanzibar bila wazanzibari wenyewe.
Mhe. Othman amefahamisha
kwamba suala hilo la mchakato wa katiba ni fursa muhimu kwa wazanzibari katika
kuyasemea na kutetea mambo muhimu yanayohusu Zanzibar ndani ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba fursa hiyo ilishindikana mwaka 2014.
Mhe. Othman amesisitiuza
kwamba hatua itasaidia sasa kupatikana
kwa Zanzibar mpya yenye mamlaka kamili ambayo ndio utajiri wa nchi katika
kufikia malengo mbali mbali ya
kimaendeleo kupitia uwezo wa kuamua na kutekeleza masuala ya miradi mbali mbali
kwa maslahi ya nchi.
Akizungunzia suala la
Muuungano na Mamlaka ya nchi Mhe. Othman, amesema kwamba hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kupiga
hatua bila ya kuwepo mamlaka na kwamba suala hilo la mchakato wa katiba
liwauanganishe wazanzibari katika kutetea wanayoyahitaji kuwepo ndani ya
Muungano.
Amefahamisha kwamba ni
vyema wazanzibari wote kuhakikisha
kwamba nchi inaingia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa na katiba mpya
yenye kuzingatia maslahi ya pende mbili muungano wenye haki na maslahi sawa kwa pande
zote mbili.
Naye Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Chama hicho , Ismail Jussa Ladhu amesema kwambna ni muhimu nchi
kuendesha shughuli zake mbali mbali katika kuzingatia taratibu zilizowekwa
pamoja na kuwepo uwazi katika masuala mbali mbali yanayotekelezwa kwenye miradi ya maendeleo ya nchi.
Aliwataka wananchi
kuelewa kwamba ACT ni chama
kilichodhamiria kuleta mabadiliko yakweli
katika kutetea maslahi ya wazanzibari na kuleta maendeleo ya Zanzibar mpya wanayoihitaji
wananchi.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha Habari leo tarehe 28.05.03.
No comments:
Post a Comment