Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Angellah Kairuki(wa pili kushoto), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (wa pili kulia)na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (kulia)wakikagua ramani ya eneo lililowekwa vigingi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wakati wa Ziara ya Kikazi ya ya kusikiliza kero za wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi.
Serikali
imewataka wananchi Wilayani Tarime Mkoani Mara kuheshimu maeneo ya Hifadhi kwa
kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema hayo leo katika
kijiji cha Gibaso Kata ya Kwihancha wakati wa ziara ya Mawaziri Watatu kutoka
Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya
kusikiliza kero za wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Serengeti.
Amesema
kuwa mwananchi yeyote haruhusiwi kukanyaga hifadhini, kutokana na kuwepo kwa
wanyama wakali na changamoto za majangili
"Nimesikia
hapa kuna malalamiko mengi pindi mnapoingia ndani ya Hifadhi, Naomba kuwaeleza
kuwa
eneo lile
linatunzwa kwa sheria za nchi na hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za
kibinadamu" Mhe. Masanja amesisitiza.
Aidha,
amefafanua kuwa kazi ya Askari wa Uhifadhi walio katika maeneo ya Hifadhi ni
kulinda Hifadhi pamoja na rasilimali zilizomo hifadhini na si vinginevyo.
Amewaasa
wananchi hao kuacha tabia ya kuwalaumu Askari Uhifadhi na badala yake waheshimu
sheria za nchi kwa kuacha kuingia katika maeneo hayo
Mhe.
Masanja amewataka wananchi kukaa katika maeneo ya vijiji yanayoruhusiwa kwa
shughuli za kibinadamu.
"Kaeni
kwenye maeneo yanayoruhusiwa yaacheni maeneo ya hifadhi yahifadhiwe na
wataalamu waliokasimiwa madaraka na Serikali" Mhe. Masanja amesema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Angellah Kairuki(wa tatu kushoto), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (wa nne kushoto)na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (wa pili kuli) wakiwa wameongozana na baadhi ya viongozi na watendaji kukagua kigingi kikuu kinachotenganisha Kijiji cha Gibaso na Hifadhi ya Taifa Serengeti wakati wa Ziara ya Kikazi ya ya kusikiliza kero za wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Gibaso Kata ya Kwinhancha wakati wa ziara ya Kikazi ya Mawaziri Watatu ya kusikiliza kero za wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Wilayani Tarime Mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Tarime wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Gibaso Kata ya Kwinhancha wakati wa ziara ya Kikazi ya Mawaziri Watatu ya kusikiliza kero za wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Wilayani Tarime Mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Angellah Kairuki (kulia), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (katikati) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (kushoto) wakijadili jambo katika Kijiji cha Kegonga wakati wa Ziara ya Kikazi ya ya kusikiliza kero za wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi Wilayani Tarime.
No comments:
Post a Comment