Habari za Punde

Vikosi Vya SMZ Kuongoza Zaezi la Uchangiaji Damu Zanzibar *CHANGIA DAMU ,CHANGIA MAZAO YA DAMU, CHANGIA MARA KWA MARA*

Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharib

Na Rahma Khamis Maelezo           15/6/2023

Waziri wa nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Mhe, Masoud Ali Mhammed amevitaka Vikosi vya SMZ kuendelea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu katika jamii.
Akizungumza mara baada ya kuzindua zoezi la  uchangiaji damu katika Uwanja wa Magirisi Melinne Wilaya ya Magharib B  ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya uchangiaji damu Duniani amesema damu ni muhimu  kwa mwanadamu kwani bila ya damu hakuna uhai .
Amesema azma ya  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Sekta ya Afya nchini hivyo uchangiaji wa Damu  unaofanywa na Vikosi hivyo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika  kuimarisha Afya za Wananachi.
 Waziri Masoud amefahamisha  kuwa damu ni muhimu katika maisha ya kila siku  kutokana na uhitaji wake hasa kwa  akina mama na watoto pamoja na wanaopata ajali hivyo ipo haja kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa uhai wa wengine.
  "Unapotoa damu ukampa mwengine umeshaokoa uhai kwani sadaka si tende na mali tu,  hata kuchangia damu ni sadaka tosha inayokufanya kuekeza mbele ya Mwenyezimungu na wala hupotezi, tena utapata faida duniani na akhera," alisema Waziri.
Aidha  amewashukuru vikosi na wananchi kwa ujumla kwa kuchangia damu  na kuwataka kutumia vyakula vya kuongeza damu  ili kurejesha damu hiyo na kuweza kutoa katika kipindi chengine.
Hata hivyo amevitaka vikosi hivyo kujilinda na kujiweka imara zaidi kwa ajili ya maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.
Akisoma risala ya maadhinisho ya siku hiyo  Sabra Mahamoud Ali kutoka Kitengo cha Damu Salama amesema kitengo cha damu salama kinaadhimisha siku hiyo  kwa kuendeleza kuchangia  damu salama ili kupunguza tatizo la upungufu wa damu Nchini.
Amesema Wizara ya Afya  Zanzibar kwa kushirikiana  na Wizara ya Afya Tanzania pamoja na Chama cha Mstalaba Mwekundu (redcroos) zimeanzisha   mpango wa damu salama ili kuokoa maisha ya watu
Aidha amefahamisha kuwa ili uweze kuchangia damu lazima kukidhi vigezo vinavyotakiwa ikiwemo  umri wa kuanzia miaka  18 ,uzito wa kilo  50 na wingi wa damu usiopungua  12 pamoja na kutokua na maradhi  nyemelezi ikiwemo sukari na presha .
Sabra ameeleza kuwa  takwimu zinaonesha kuwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu ni mama wanaojifungua  na  watoto hivyo ipo haja kwa jamii kuhakikisha kama ana sifa kushiriki katika kutoa damu.
Nae mchangiaji bora wa damu ambaye ameshachangia mara hamsini na sita Hassan Pandu Khamis ameipongeza Wizara kwa kumpatia zawadi na kuitaka jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia kwani  wahitaji ni wengi .
Maadhimisho ya siku ya uchangiaji wa damu Duniani hufanyika kila ifikapo juni 14 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu CHANGIA DAMU ,CHANGIA MAZAO YA DAMU, CHANGIA MARA KWA MARA.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed   akipata maelezo kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu kutoka kwa Meneja wa kitengo cha damu salama  Dkt  Masuod Ali masoud wakati alipotaka kuzindua zoezi hilo ikiwa ni maadhimisho ya  siku ya uchangiaji damu ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  Hassan Hafidh Khamis akizunguza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed  kuzindua zoezi la uchangiaji damu katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ  Massoud Ali Mohammed akizingumza na wachangiaji damu (hawamo pichani) wakati akizundua zoezi la uchangiaji damu  katika maadhimisho  ya siku ya wachangiaji damu ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 14,hafla iliyofanyika Juni 15,2023 huko  Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi.



Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed  akikamkabidhi zawadi maalum mchangiaji wa damu kundi adimu ( rhesus-) Juma Kombo Dawa wakati wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu Duniani  ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed  akimkabidhi zawadi maalum mchangiaji bora wa damu Khamis Pandu Khamis  ambae ameshachangia mara 56, wakati wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu Duniani  ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi

Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed  akisalimiana na kufurahi pamoja na Vijana wa kikosi cha Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) wakati wa hafla ya uchangiaji damu iliyofanyika uwanja wa magirisi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu duniani ambayo Kitaifa  huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi 
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na   Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed  akisalimiana na kufurahi pamoja na Vijana wa kikosi cha Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) wakati wa hafla ya uchangiaji damu iliyofanyika uwanja wa magirisi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu duniani ambayo Kitaifa  huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.