Dk. Mwinyi alitoa agizo
hilo ukumbi wa hotel ya Golden Tulip, uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi
kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa ZSSF.
Alisema, kazi kubwa inayoendelea kufanywa na ZSSF
ni mabadiliko na huduma bora kwenye sekta ya uwekezaji wa miradi mbali mbali ya
maendeleo inayogusa jamii moja kwa moja.
“Miradi yote inayotekelezwa na iliyopangwa
kutekelezwa na ZSSF sina shaka itaongeza faida kwa ZSSF, itakuza uchumi na
kutoa fursa nyingi za ajira nchini” Alisifu Rais Dk. Mwinyi.
Alisema, ZSSF inatokana na ushirikiano baina ya
Serikali, Waajiri na Waajiriwa, hivyo alizitaka taasisi za Serikali na Jumuiya
zote kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji
wa taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao
wanapostaafu au wanapohitaji mafao yao.
Pia Rais Dk. Mwinyi alizitaka Taasisi za Serikali
zishirikiane kutoa huduma ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima wananchi.
Kadhalika, aliwaomba wajasiriliamali wajisajili ili
wachangia kwenye Mfuko wa hiari kwani una faida hasa pale biashara zao zitakapotetereka
au watakapohitaji mafao ya aina yoyote.
Akitoa ushuhuda kwa mataifa yaliyoendelea duniani,
Rais Dk. Mwinyi alieleza lengo la kuanzishwa kwa sekta za huduma za jamii ni kukusanya
michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Aidha, alieleza
Sekta hiyo pia hutumika kuinua uchumi wa nchi na wananchi hasa kwenye uwekezaji
wa miradi mikubwa yenye tija.
Alisistiza, Sekta
ya hifadhi ya jamii ni nguzo muhimu ya uchumi inayotegemewa na nchi pamoja na
wafanyakazi.
Alieleza licha ya
mafanikio makubwa ya ZSSF ndani ya miaka 25 tokea kuanzishwa kwake, lakini bado
haijawekeza kwenye miradi mikubwa zaidi, hivyo, aliieleza taasisi hiyo ina
wajibu wa kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufanisi kwenye uwekezaji wenye
tija zaidi.
Pia, aliipongeza
ZSSF kwa utekelezaji wa agizo lake la kuongeza pensheni kwa wastaafu wa kima
cha chini kutoka shilingi 90,000 hadi 180,000 kama Serikali ilivyoongeza kwa
wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza malifakutoa mafao kwa
wastaafu lakini pia ZSSF imegusa hudua zote za jamii zikiwemo, Afya michezo,
elimu vituo vya daladala na huduma
nyengine kwa wananchi.
Naye, Mkurugenzi
Mwendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Nassor Shaaban, alieleza lengo
la kuunzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa ulinzi na kinga kwa wanachama wake kwa
kutoa pencheni na mafao mbalimbali.
Akizungujmzia mafanikio
ya ZSSF kwa kipindi cha miaka miwili ya Dk Mwinyi alieleza ni pamoja na utekelezaji
wa Ilani ya CCM ya 2025 nakuonengeza hadi sasa Mfuko umetekeleza miradi ya
maendeleo kwa asilimia 90, pamoja na kutekeleza jukumu la kisheria la mfuko
ikiwemo kusajili mwanachama, uwekezaji pamoja na ulipaji wa mafao na pencheni.
Miongozi mwa mafao
yanayotolewa na ZSSF ni pamoja fao la kustaafu, uzazi, fao la wenye ulemavu,
kuumia kazini na fao la wajasiriamali. ZSSF ilianzishwa rasmi mwaka 1998, maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi
hiyo yalikwenda sambamba na kauli mbiu, “Nidhamu, Uwajibikaji teknolojia
ya sasa na uwekezaji endelevu na mafao bora kwa wanachama”.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment