Al hajj Dk. Mwinyi, alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti
wa Ijumaa Miembeni Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuika pamoja na waumini wa
dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa.
Rais, Al hajj Mwinyi,
aliieleza jamii
kadri inavyokusanyika pamoja kwenye shughuli mbalimbali za maisha ya kila siku,
wasichoke kuhimizana umuhimu wa amani ya nchi, kwani kufanya hivyo ni kutimiza
malengo mazuri waliyoyakusudia ya ustawi wa jamii bora na maendeleo ya uchumi.
“Haya yote
tunayoyafanya, yawe ya maendeleo, jamii au ibada misikitini yanategemea amani
ya nchi” Alisisitiza Al hajj Dk. Mwinyi.
Al hajj Dk. Mwinyi alieleza
umoja na mshikamano wa jamii ndio msingi wa kufikia malengo iliyojiwekea, kwa
ajili ya maendeleo ya Zanzibar”.
Hata hivyo, aliwataka
waumini hao waendelee kuombeana du’a na kuliombea taifa katika kufanikisha
maleongo yake.
Akihutubu kwenye sala
hiyo, Khatibu Sheikh Khalid Ali Mfaume alieleza umuhimu wa siku ya Ashura kwenye historia ya
uislam na kusisitiza jamii ya waislam
kuendelea kukithirisha ibada hasa kwenye mwezi mtukufu wa Muharam.
Sheikh Khalid ambae pia ni Katibu Mtendaji kutoka
Ofisi ya Mufti Zanzibar, alisema, Mwezi
wa Mfunguo nne (Muharami) ni miongoni mwa miezi minne mitukufu ya Mwenyezi
Mungu kwenye kalenda ya uislam pia alieleza mwezi 10 Muharam ni sunna kufunga funga
ya Ashura kwa waumini wa dini ya kiislam.
Alisema, funga hiyo ni
bora baada ya Ramadhani ambayo Mtume (SAW) aliifunga mara baada ya kuhamia
Madina.
Hivyo, aliihimiza jamii
ya waislam kuzitumia vyema siku tukufu za mwezi wa Muharam kwa kuendelea
kukithirisha ibada na kuacha mabaya yote aliyoyakata Mwenyezi Mungu (S.W).
Mara baada ya sala ya
Ijuma, Rais Al hajj Dk. Mwinyi alimtembelea kwa kumjuulia hali Bi. Khadija
Abass Rashid, mkaazi wa Rahaleo Wilaya ya Mjini alieshiriki kwenye tukio
la historia la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 wakati
wa kuasisiwa kwa taifa la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment