Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akishiriki Mkutano wa 19 wa Baraza ka
Mawaziri wa Mazingira wa Afrika wenye lengo la kuandaa misimamo ya bara hilo
kwenye masuala mbalimbali ya kimazingira, unaoendelea jijini Addis Ababa nchini
Ethiopia leo tarehe 17 Agosti, 2023
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
ameongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa 19 wa Baraza ka Mawaziri wa Mazingira
wa Afrika unaoendelea jijini Addis Ababa nchini Ethiopia leo tarehe 17 Agosti,
2023.
Mkutano huo unaofanyika kila mwaka na kuhusisha viongozi hao kutoka mataifa mbalimbali barani humo, unalenga kujadili changamoto za mazingira zinazozikabili nchi za Afrika.
Akizungumzia mkutano huo, Naibu Waziri Khamis amesema nchi hizo zinakutana pia kuandaa misimamo yao kwenye masuala mbalimbali ya kimazingira.
Aidha,
amebainisha kuwa viongozi wanafanya maandalizi na kuweka misimamo ya pamoja kuelekea
Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi (COP 28) unaotarajiwa kufanyika Falme za Kiarabu pamoja na ule wa Baraza
la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka.
Mhe. Khamis ameongeza kuwa manufaa ya mkutano huo ni kupeana uzoefu na wataalamu wengine kutoka Afrika kwenye masuala mbalimbali ya kimazingira.
No comments:
Post a Comment