Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ajumuika na waumini katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Bomani Baja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi, alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Bomani Baja Wilaya ya Mjini Unguja kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 11-8-2023, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe. Rashid Simai Msaraka.
BAADHI ya Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo leo 11-8-2023.
BAADHI ya Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo leo 11-8-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika katika Msikiti wa Bomani Baja Wilaya ya Mjini Unguja leo 11-8-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Dini, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Bomani Baja Wilaya ya Mjini Unguja leo 11-8-2023.
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameihimiza jamii kuendeleza malezi bora kwa watoto na vijana ili kulinusuru Taifa na mporomoko wa maadili.

Al Hajj Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti wa Polisi Bomani, Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa.

Alisema, siku hizi maadili yamepotea, jamii zimekithiri vitendo visivyo na maadili mema kwa vijana ikiwemo wizi, watumiaji wa dawa za kulevya, tofauti na zamani, hivyo aliwahimiza wazazi/walezi kuwalea vijana kwa hofu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu (S.W).

Alieleza, ndani ya jamii kuna mmong’onyoko wa maadili, hivyo aliendelea kuiasa jamii kushirikiana kwenye malezi ya pamoja ili kuwanusuru vijana na janga hilo.

Alieleza wazazi/ walezi wanawajibu wa kuhakikisha makosa na mporomoko wa maadili hayafanyiki kwa vijana wao kwa kuendelea kuwa wasimamizi wazuri kwao badala ya kusubiria vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kisheria, hivyo aliwahimiza kuendelea kuchukua tahadhari mapema.

Katika hatua nyengine, Al hajj Dk. Mwinyi aliisa jamii kuendelea kuvumiliana na kuendeleza amani ya nchi licha ya tofauti za kisiasa na imani zilizopo.

Alisema, ndani ya nchi yenye watu wenye mitazamo na fikra tofauti haiwezekani wote wakakubaliana kwa kila jambo, lakini kikubwa katika hayo ni kuvumiliana na kuelewana.

Aidha, Al hajj Dk. Mwinyi aliwaomba wanasiasa wa vyama mbalimbali kupitia viongozi wa dini na waumini wao, kuendelea kubakia na amani na uvumilivu kwani wakati mwengine kumekua kukijitokeza viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutovumiliana kwenye jamii.

Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendelea kumuombea na kumtakia kheir Al hajj Dk. Mwinyi kwani tokea ameingia madarakani maekua na ushirikiano mkubwa kwenye jamii kwa kuendeleza utaratibu wake wa kushirikiana na jamii kwenye masuala ya khairati ikiwemo kujumuika nao pamoja kwa sala za Ijumaa kupitia misikiti ya maeneo mbalimbali ya nchi.

Akihutubu kwenye sala hiyo, Khatibu Sheikh Salum Othman Malolo aliiasa jamii kujiepusha na zinaa ya macho kwa kuangalia na ya ulimi kwa kutamka machafu na kusifia maovu yanayofanyika kwenye jamii. Hivyo aliitaka jamii kutozingatia na kujiepusha kutamani masuala machafu ya zinaa.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.